top of page

Hubirini Kwa Sauti


Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya Hubirini kwa sauti ya kinanda, tangazeni haya Yatamkeni, tamkeni hadi mwisho wa dunia Semeni Bwana amelikomboa taifa lake

  1. Mwimbieni Bwana wimbo ule mpya, mwimbieni Bwana enyi mataifa mwimbieni Bwana kwa sauti ya shangwe, Mwimbieni Bwana libarikini jina lake

  2. Tangazeni wokovu siku kwa siku, hubirini habari za utukufu yahubirini mataifa sifa zake, na watu wote habari za ukuu wake

  3. Mpeni Bwana utukufu na nguvu, mpeni Bwana enyi wana wa Mungu, pelekeni habari zake pande zote, Mpeni Bwana utukufu wa jina lake

  4. Mwabuduni Bwana kwa utakatifu, tetemekeni mbeleze nchi yote semeni kwamba Bwana ametamalaki, atawahukumu watu wake kwa adili

3 views0 comments

Commentaires

Noté 0 étoile sur 5.
Pas encore de note

Ajouter une note
bottom of page