top of page

Hosana Juu Mbinguni

1. Nani atakayepanda kwenye mlima wa Bwana, nani ‘takayesimama kwenye hekalu la Bwana.

Hosana juu mbinguni x5. Nani atakayepanda kwenye mlima wa Bwana? Patakatifuni pake nani ‘takaye simama?

2. Yule atendaye mema, na moyo wake ni safi, hashuhudii uongo wala kuapa kwa hila.

3. Yeye atazipokea baraka kwake Mwenyezi, kwake Mungu wa wokovu haki ataipokea.

4. Hiyo ni hali ya watu wamtafutao Mwenyezi, hali ya wanaofika kwa Mungu wa Yakobo.

5. Haya, fungukeni sasa , enyi milango ya kale, ili Mfalme Mtukufu hima apate ingia.

6. Ndiye mwenye utukufu, na sifa, na enzi, Mungu hodari vitani, yeye ni mwenye uwezo.

7. Ndiye aliyeijenga dunia juu ya bahari, na kuiweka imara juu ya mito ya maji.

8. Dunia na vilivyomo ni mali yake Mwenyezi, nao waishio humo ni mali ya Mungu wetu.

10 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page