top of page

Hodi Hodi Nyumbani Mwako Bwana


Hodi hodi nyumbani mwako Bwana, ninabisha nifungulie Nimekuja nyumbani mwako leo, nimekuja kukuabudu, Kwa unyenyekevu naijongea, meza yako yenye baraka Nakuja na sala zangu Ee Bwana, nakuomba zisikilize Ninakutolea sadaka safi, Mungu Baba uipokee.

  1. Nyua za Bwana zapendeza, zinapendeza macho kama nini (Natamani kuingia hekaluni, nikamwabudu) x2

  2. Nimeingia hekaluni, nimeingia hekaluni mwako (Nimekuja kuabudu kusujudu, nyumbani mwako) x2

  3. Unipokee Mungu wangu unitakase, mimi mwenye dhambi (Nimekuja mbele zako Mungu Baba, unipokee) x2

13 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page