top of page

Hii ni Karamu

Hii ni karamu uzima wa roho, yumo Bwana Yesu, kwa mwili wake kweli na damu yake.

1. Alisema Bwana twaeni wote mle ni mwili wangu.

2. Alisema Bwana twaeni wote mnywe ni damu yangu.

3. Nasi twasadiki ni mwili wake kweli na damu yake

4. Alituamuru kufanya hivyo kwa ukumbusho wake.

5. Tukifanya hivyo tunatangaza kifo cha Bwana wetu.

6. Kwa hii karamu twashiriki uzima wa Bwana wetu.

7. Huu ni upendo aliotuachia Mkombozi wetu.

8. Hapa duniani twaishi na Baba kwa karamu hii.

9. Na huko mbinguni tutaishi na Baba milele yote.

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page