top of page

Hii ni Ekaristi



  1. Hii ni Ekaristi aliyotuachia, Bwana Yesu Kristu, Kristu, Mkombozi wa dunia. Imbeni, imbeni kwa furaha,sifuni, sifuni Ekaristi, alimo Yesu Kristu, Kristu, alimo ni mzima.

  2. Yesu katuonea, wema pia huruma, alitupenda sana, sana akatupa uzima.

  3. Jioni Alhamisi, alichukua mkate, kaugeuza mwili mwili, kuleni mkaokoke.

  4. Pia alichukua, kikombe cha divai, kaigeuza damu,damu,kunyweni mkaokoke.

  5. Walipokwisha kula,kawaosha miguu nimewapa mfano, mfano, fanyeni nanyi vile.

  6. Yesu mwili na damu, chakula cha mbinguni, tujaliwe kupata, pata, uzima wa milele.

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page