top of page

Heri yenu Mungu Amewaunganisha

Heri yenu Mungu amewaunganisha, msitengane, mkavunja hili agano) x2

  1. Aliumba wazazi wetu kale, paradisini waitawale.

  2. Aliumba Adamu babu yetu, na Eva mzazi wetu wa kwanza.

  3. Akasema zaeni mkaenee, ijazeni dunia na watu

  4. Leo Mungu amewabarikia, mkafunga agano tukufu.

  5. Lishikeni agano takatifu, siku zote za maisha yenu.

  6. Pete yenu kwa kweli ni mnyororo, waivaao wasiachane.

  7. Enendeni wawili tangu leo, miongoni mwa raha na taabu.

  8. Nyumba yenu ijae upendano, akosaye atubu mapema.

  9. Na amani ya wenye kumcha Mungu, iwavutie nyoyo za watu.

  10. Sioni sababu ya heshima, isiwe msingi wa maisha yenu.

  11. Za mwenyezi baraka ni watoto, muwatunze, muwalee vyema.

  12. Si watoto wa kwenu ni wa Mungu, wafundishe mapema kumpenda.

  13. Na mwishowe baada ya miaka, wote awafikishe pema

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page