top of page

Hapa We Msafiri

Hapa we msafiri simama na tazama (simama na tazama) Nimekufa leo, kesho - ni zamu yako (ona) ona vema nilivyowekwa humu, Na nilivyoacha mali na jamaa


Nilitoka uchi tumboni mwa mamangu . . . Narudia uchi, kati-ka tumbo la nchi (Sanda) sanda moja hilo ni vazi langu, Wameninyang'anya hata senti moja.


Nifunike vema na hilo jembe lako . . . Nalitangatanga, kati-ka ulimwengu (Basi) basi leo kiburi kimekwisha, Kumbe dunia hii ni mti mkavu.


Nyumba yangu leo ni shimo udongoni . . . Hakuna mlango, haku-na madirisha (Kita) kitanda changu na blanketi langu, Ni udongo mzito wanielemea


Kifafanuacho wafu mbele ya Mungu . . . Si cheo kikubwa, si da-raja si sifa (Mate-) matendo mema saa ya kufa kwangu, Yatafungua mlango wa uwingu


Ole wangu mimi nilifanya ujinga . . . Kwa kuambatana, na wa-tu wa dunia (Ona) ona wote leo wameniacha, Hasa watu wale niliowapenda.


Unapojiona jiwazie mwenyewe . . . Kufa siku moja, kwa wo-te ni lazima (Japo) japo sultani japo ni mtumwa, Mungu atamwita ikiwa saa yake.


Nimekufa leo nilipona salama . . . Nalijidhania, mwenye - afya mwilini (na ma-) na mara moja nikaanguka chini Labda huamini kwamba nali`mzima.


Yesu msalabani kateswa vikali mno . . . Kwa kutukomboa, aka-mwaga damuye Wahurumie wote wa toharani, Mwanga wa milele uwaangazie.


Kwaherini wote kwaherini wapenzi . . . Ninakwenda kwetu sita-rudi nyuma (Kwa he-) Kwaheri Baba kwaheri Mama yangu, Mungu akipenda kwake tukutane.

5 views0 comments

Comentarios

Obtuvo 0 de 5 estrellas.
Aún no hay calificaciones

Agrega una calificación
bottom of page