top of page

Guadalupe Mass

BWANA UTUHURUMIE.

Bwana tuhurumie tuhurumie,Bwana, Bwana,Bwana ee Bwana ee, Bwana tuhurumie x2

Kristu tuhurumie…..

Bwana tuhurumie….


UTUKUFU


Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu, tunakutukuza x2


Utukufu kwa Mungu juu Mbinguni na amani duniani kwa watu wa mapenzi mema tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu


Ee Mungu Mfalme wa mbinguni Baba Mwenyezi / ewe

Bwana wetu Yesu Kristu Mwana wa pekee.


Ee Bwana wa Mungu wa Mwana Kondoo wa Mungu, Mwana wake Baba mwenye kuondoa dhambi za watu.


Ewe Mwenye kuondoa dhamb za dunia Mungu, utuhurumie ombi letu upokee.


Ewe Mwenye kuketii kuume kwa Baba mwenyezi, utuhurumie ndiwe Peke yako Mtakatifu.


Pekee yako ni Mwana wa Pekee Mkuu Yesu Kristu, pamoja na Roho katika utukufu wa Mungu Baba.


NASADIKI

Nasadiki kwa Mungu mmoja Muumba mbingu na dunia na kwa

mwana wa pekee yesu Kristu Bwana wetu ninasadiki


Aliyetungwa kwa uwezo wake Roho Mtakatifu kazaliwa na Bikira ninasadiki


Aliteswa kwa pilato alisulibiwa na akafa akazikwa akashukia na kuzimu kafufuka yeye siku ya tatu toka wafu ninasadiki


Ninasadiiki, ninasadiki, ninasadiki


Akapaa juu mbinguni, ameketi kuume kwake Baba mwenyezi

Atakapotokea kuhukumu watu wote wazima na wafu


Nasadiki kwake Roho na kanisa takatifu katoliki la mitume

Ushirika ule mwema wa watakatifu wote, maondoleo ya dhambi


Ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo Amina


MTAKATIFU

Mtakatifu, mtakatifu

Mtakatifu Bwana, Bwana Mungu Bwana Mungu wa majeshi.

Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako mbingu na dunia zimejaa utukufu wako Bwana


Hosanna x 7 (Juu mbinguni)


Mbarikiwa anayekuja Kwa jina la Bwana Bwana Mungu wa majeshi


BABA YETU

Baba yetu (Baba) wa mbinguni, jina lako litukuzwe, Baba yetu wa mbinguni (na) jina lako litukuzwe


Falme wako utufikie, utakalo na alifanyike– Jina lako litukuzwe

Duniani kama mbinguni, duniani kama mbinguni- Jina lako litukuzwe


Tupe leo mkate wetu, mkate wetu wa kila siku -

Tusamehe makosa yetu, tusameheavyo watukoseao -


Situtie kshawishini walakini utuopoe –

Tuopoe kwenye maovu, tuopoe kwenye maovu –


Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu –

Utukufu hata milele, utukufu hata milele –


MWANAKONDOO

Mwanakondoo wa Mungu,

Mwana, mwana, uondoaye dhambi za dunia, mwana (Ee) mwana (Ee) Mwana tuhurumie x2

Mwanakondoo wa Mungu, mwana, mwana, uondoaye dhambi za dunia, mwana (A/Ee) mwana, utujalie amani, utujalie amani, amani.

116 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page