top of page

Fransiscan Mass


BWANA ‘TUHURUMIE’


Bwana tuhurumie, Bwana tuhurumie, Bwana tuhurumie ee Bwana, ee Bwana…

Kristu tuhurumie, Kristu tuhurumie ,Kristu tuhurumie ee Kristu, ee Kristu tuhurumie

Tuhurumie;

Bwana tuhurumie……… (endelea kama mwanzo)


UTUKUFU


1. Tenor: Kwake utukufu Mungu juu mbinguni,

Sop: Na kote amani hapa duniani

Wote: Kwa wote watu wa mapenzi mema).

Sop/Alto: Tunakushukuru Mungu kwa ajili

Wote: Ya utukufu wako ule mkuu.

KIITIKIO: Tunakusifu, (Bwana) tunakuheshimu, tunakuabudu (Bwana) tunakutukuza.x2

2. Tenor: Ewe Bwana Mungu Mfalme wa mbinguni,

Wote: Ni wewe Mungu Baba Mwenyezi

Sop/Alto: Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee

Wote: Ee Bwana Mungu Mwana wa Baba.

3. Tenor: Mwenye kuondoa dhambi za dunia,

Wote: Ee Bwana Yesu utuhurume.

Sop/Alto: Mwenye kuondoa dhambi za dunia,

Wote: Ee Yesu we pokea ombi letu.

4. Tenor: Mwenye kuketi kuume kwa Baba,

Wote: Wetu Mwokozi utuhurumie.

Sop/Alto: Pekee yako Bwana ndiwe Mtakatifu,

Wote: Na pekee yako mkuu Yesu Kristu.

5.Tenor Pamoja na yeye Roho Mtakatifu,

Wote: Kwa utukufu wake Mungu Baba.

Sop/Alto Pamoja na yeye Roho Mtakatifu,

Wote: Kwa utukufu wake Bwana Baba.



NASADIKI


1. Tenor: Nasadiki kwa Mungu mmoja kwa Mungu mmoja, muumba mbingu na dunia na kwa Mwana wa pekee, Yesu Kristu

Bwana wetu, ( Nasadiki) Alitungwa kwa uwezo wake Roho Mtakatifu, kazaliwa na Bikira.

Kiitikio: (T) Nasadiki. (W) Nasadiki –I Kweli nasadiki.

2. Aliteswa kwa Pilato pia alisulibiwa, na akafa akazaliwa, akazikwa, kashukia na kuzima kafufuka yeye siku ya tatu toka kwa

wafu.

3. Akapaa juu mbinguni ameketi kuume kwake Baba Mwenyezi, atakapotokea kuhukumu watu wote wazima na wafu.

5. Nasdiki kwa Roho Mtakatifu na kanisa takatifu katoliki la mitume, ushirika ule mwema wa watakatifu wote, maondeleo ya

dhambi zetu, ( ufufuko wa miili na uzima wa milele, ijayo A-mina) x 2


MTAKATIFU


Mtakatifu (Mtakatifu)Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi

Mbingu na dunia, mbingu na dunia kweli zimejaa utukufu wako.

Hosanna juu Hosana juu mbinguni, Hosanna juu Hosana juu mbinguni x2

Mbarikiwa anayekuja, na kwa jina lake Mungu wa majeshi x 2


FUMBO LA IMANI


Ee Bwana-a -kila tunapo kula mkate huu, na kunywa kikombe hiki, Tunatangaza kifo chako-o

mpaka utakapo kuja .

BABA YETU


Baba yetu wa mbinguni jina lako litukuzwe, ufalme wako na, ufike utakalo lifanyike x 2


1. Duniani kama mbinguni- Baba ee Baba yetu;

Tupe leo mkate wetu……. Mkate wetu wa kila siku……..


2. Tusamehe makosa yetu……. Kama vile twawasamehe ……… waliotukosea sisi

3. ……. Situtie kishawishini…….. walakini utuopoe…….. maovuni utuopoe……..


4. Kwa kuwa ufalme ni wako….. na nguvu na utukufu….. utukufu hata milele…..


MWANAKONDOO WA MUNGU


Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia, tuhurumieutuhurumie x 2


2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page