top of page

Fadhili Mass

BWANA UTUHURUMIE.

Tenor: Bwana, Bwana utuhurumie ee Bwana

All: Bwana, Bwana, Bwana utuhurumie.

Tenor: Kristu, Kristu utuhurumie ee Kristu

All: Kristu, Kristu, Kristu utuhurumie.

Tenor: Bwana, Bwana utuhurumie ee Bwana

All: Bwana, Bwana, Bwana utuhurumie.



UTUKUFU:

Tenor: Utukufu kwa Mungu mbinguni

All: Utukufu kwako Mungu mbinguni

Na amani pote duniani

Kwao watu wa mapenzi mema.

1. Tunakuheshimu, tunakusifu, tunakuabudu, twakutukuza ee Bwana.

2. Tunakushukuru, Mfalme wa mbinguni, Mwana wa pekee, Mwana wa Baba ee Bwana.

3. Unayeondoa makosa yetu, utuhurumie,’tusikilize ee Bwana.

4. Kuume kwa Baba unapoketi, Mtakatifu mkuu ‘tuhurumie ee Bwana.

5. Roho mtakatifu pamoja nawe, ndani yake Baba unatukuzwa ee Bwana.


NASADIKI:

1. Nasadiki kwa Mungu Baba, Muumba wa vyote, Nasadiki kwa Yesu Kristu Mwana wa pekee.

Nasadiki, ninasadiki x2

2. Kwa uwezo wa Roho Mungu ‘katwaa mwili, na hapo Bikira Maria ‘kawa mamaye.

3. Kwa amri ya Ponsyo Pilato kasulubiwa, Akafa,’kazikwa, akashukia kuzimu.

4. Siku ya tatu ‘kafufuka ‘kapaa mbinguni, Kaketi kuume kwa Mungu Baba mwenyezi

5. Atarudi siku ya mwisho kutuhukumu, Nasadiki kwa Roho mfariji Mtakatifu.

6. Kanisa pia takatifu na Katoliki, Ushirika wa Watakatifu wa mbinguni.

7. Na maondoleo ya dhambi kwa ubatizo, ‘fufuko wa miili, uzima wa milele.


MTAKATIFU.

Mtakatifu, Mtakatifu Bwana Mtakatifu Mungu wa majeshi

Mbingu na dunia zimejaa, zimejaa utukufu wako

Hosana, Hosana, Hosana, Hosana, Hosana,

Hosana juu mbinguni x2

Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina lake Bwana


FUMBO LA IMANI.

Ee Bwana tunatangaza kifo chako,

Na kutukuza ufufuko wako

(Mpaka utakapo kuja)x2


BABA YETU.

Jina lako Baba litukuzwe, utawale petu milele yote x2

1. Baba yetu mwema, uliye mbinguni, Jina lako Baba litukuzwe

2. Na ufalme wako, uje hapa kwetu, Na mapenzi yako yatimilike.

3. Tupe leo mkate, wa kila siku, Tupe leo mkate, wa kila siku

4. Na utusamehe, makosa yetu, Kama tufanyavyo kwa ndugu zetu

5. Situtie Baba kishawishini Bali maovuni utuopoe.

6. Ufalme na nguvu, na utukufu, Vyote vyako Baba, hata milele.


MWANA KONDOO.

Mwanakondoo wa Mungu

Unayeondoa dhambi za dunia, ee Bwana

Tuhurumie, tuhurumie x2

Mwanakondoo wa Mungu

Unayeondoa dhambi za dunia, ee Bwana

Utujalie amani.

14 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page