top of page

Enyi Wakristu Wapenzi



Enyi wakristu wapenzi, njoni Bwana anatualika kwenye karamu x 2. kwanza (ndugu) tazama, meza yake inavyo pendeza (yeye). Bwana na wateule, wameizunguka meza yake. (Haya ndugu simama nawe ushiriki x 2)

  1. Njooni Bwana atuita, meza yake sasa itayari, haya simama, nenda nawe ushiriki.

  2. Kama wewe wastahili, fanya hima ukampokee, ndicho chakula, chenye uzima milele.

  3. Yeye anilae mimi, atakuwa na uzima mpya, siku ya mwisho, mimi nitamfufua.

  4. Yeye 'katuandalia, masikini pia matajiri, ukarimu gani Bwana Yesu anayo.

10 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page