top of page

Ee Mpendwa wa Nafsi Yangu

Ee mpendwa wa nafsi yangu, usimame nawe ujipambe, mavazi yako mazuri (kisha) twende hekaluni nikathibitishe kwamba mimi nakupenda

Duniani kuna mambo, kuna wengi kuna mengi

Kati yao wengi nayo mengi mimi nimekuchagua wewe.


Duniani kuna mambo, kuna shida kuna raha

Wakati wa dhiki na raha mimi nitakuwa mfariji.


Duniani kuna mambo, kuna kupeana kero,

Wakati wa penzi na mashaka mimi nitakuwa mwaminifu.


Duniani kuna mambo, kuna wengi mwafanana,

Kiapo nilicho apa leo mimi ndiyo hukumu yangu.

9 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page