top of page

Dunia Hii

Dunia hii kitu gani kwangu, sioni heri niuchungu tupu. Nayatamani maisha ya mbingu, niishi nawe Yesu wangu mwema.


1a. Ni kwambie nini Yesu wangu,ujue ya kwamba nakupenda.

b.Hakuna chochote duniani,chenye kufariji moyo wangu.


2a. Sina mamlaka ya pumzi yangu,ikiwezekana nichukue.

b.Sio kwa mapenzi yangu mimi,bali kwa mapenzi yako wewe.


3a. Ndani ya mapendo ni furaha,na ndani yake huja kilio,

b.Ndani ya ukiwa ni mateso, mwisho huja furaha mbingu

12 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page