top of page

Cha kutumaini Sina

Cha kutumaini sina, ila damu yake Yesu,

sina wema wa kutosha, dhambi zangu

kuziosha, kwake Yesu nasimama

Ndiye mwamba ni salama x3


Njia yangu iwe ndefu, yeye hunipa wokovu

Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndizo nanga

Kwake Yesu nasimama

Ndiye mwamba ni salama x3


Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani

Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele

zake, kwake Yesu nasimama

Ndiye mwamba ni salama x3


Damu yake na sadaka, nategemea

daima, yote chini yakiisha, Mwokozi

atanitosha, kwake Yesu nasimama

Ndiye mwamba ni salama x3

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page