top of page

Centenary Mass

Utuhurumie ee Bwana, ee,

Ee Bwana, ee Bwana


Utuhurumie ee Bwana, ee,

Ee Bwana, ‘tuhurumie.

Utuhurumie ee Bwana, ee,

Ee Bwana, ee Bwana


Utuhurumie ee Bwana, ee,

Ee Bwana, ‘tuhurumie.


Ee Kristu, ‘tuhurumie, ‘tuhurumie,

Utuhurumie ee, ee Kristu ‘tuhurumie,

Ee Kristu ‘tuhurumie.


Utuhurumie…


UTUKUFU

Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, Na amani iwe kwa watu wenye Mapenzi mema duniani kote.


Tunakusifu, Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu,

tunakutukuza.


Tunakushukuru, Mungu kwa ajili, Ya ‘tukufu wako mkuu, ee Bwana, ni Mungu ndiwe Mfalme wa mbinguni


Ee Baba Mwenyezi, Bwana Yesu Kristu, Ee Mwana wa pekee, ee Mungu Mwana Kondoo wa Mungu, Mwana wake Baba.


Mwenye kuondoa dhambi za dunia, Utuhurumie, ‘tuhurumie,

Maombi yetu, Bwana, uyapokee.


Mwenye kuketi kuume kwa Baba, Utuhurumie, kwa kuwa ndiwe

Pekee yako ni Mtakatifu


Pekee yako, Bwana, pekee yako mkuu, Ewe Yesu Kristu, pamoja naye Roho Mtakatifu milele yote.


NASADIKI

Nasadiki kwa Mungu Mmoja- Nasadiki

Ndiye Baba yetu Mwenyezi- Nasadiki

Muumba mbingu pia dunia- Nasadiki

Nasadiki kwa Yesu Kristu- Nasadiki


Nasadiki Nasadiki (Nasadiki) Nasadiki, Nasadiki.


Mwana wa pekee wa Mungu- Nasadiki

Aliyezaliwa kwa Baba- Nasadiki

Akapata mwili Roho- Nasadiki

Kazaliwa naye Bikira- Nasadiki


Nasadiki Nasadiki (Nasadiki) Nasadiki, Nasadiki.


Kisha yeye ‘kasulibiwa- Nasadiki

Kwa amri ya Pilato-Nasadiki

Kwa ajili yetu ‘kateswa- Nasadiki

Akafa na akazikwa- Nasadiki


Nasadiki Nasadiki (Nasadiki) Nasadiki, Nasadiki.


‘Kafufuka katika wafu- Nasadiki

Akapaa juu mbinguni- Nasadiki

Ameketi kuume kwake- Nasadiki,

Mungu Baba wetu Mwenyezi- Nasadiki,


Nasadiki Nasadiki (Nasadiki) Nasadiki, Nasadiki.


Ndipo atakapotokea- Nasadiki

Kuhukumu wazima na wafu-Nasadiki,

Kwake Roho mtakatifu-Nasadiki

Kwa kanisa la katoliki- Nasadiki


Nasadiki Nasadiki (Nasadiki) Nasadiki, Nasadiki.


Ushirika wa watakatifu- Nasadiki

Ondoleo la dhambi zetu- Nasadiki

Nangojea ‘fufuko wa mwili- Nasadiki

Na uzima wa milele- Nasadiki


MTAKATIFU

Mtakatifu, mtakatifu,

Mtakatifu, Bwana Mungu.


Mtakatifu, mtakatifu,

Mtakatifu Bwana Mungu, wa majeshi, x2


Mbingu na dunia zimejaa utukufu

Mbingu na dunia, mbingu na dunia,

Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako,

Zimejaa utukufu wako.


Hosana juu, hosanna juu,

Hosana juu, hosanna juu mbinguni x2


Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina

Mbarikiwa yeye, mbarikiwa yeye,

Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana,

Ajaye kwa jina la Bwana.


Hosana juu, hosanna juu,

Hosana juu, hosanna juu mbinguni x2



FUMBO LA IMANI

Yesu Kristu alikufa

Yesu Kristu alikufa,

Yesu Krisu alifufuka

Yesu Kristu atakuja kwetu tena x2


BABA YETU

Baba yetu wa mbinguni, (Baba),

Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike,

(Baba) utakalo lifanyike}x2


Duniani kama mbinguni, Baba- Utakalo lifanyike

Tupe leo mkate wetu, Baba- Utakalo lifanyike


Mkate wetu wa kila siku, Baba- Utakalo lifanyike

Tusamehe makosa yetu kama vile tunavyo wasamehe waliotukosea sisi- Utakalo lifanyike.


Situtie kishawishini, Baba -

Walakini utuopoe, Baba -

Maovuni utuopoe,Baba -


Kwa kuwa ‘falme ni wako, Baba -

Na nguvu na utukufu, Baba -

Utukufu hata milele, Baba


MWANA KONDOO

Ee Mwana kondoo wa Mungu

Uondoaye dhambi za dunia, ee

Ee Mwana ‘tuhurumie.

Mwana kondoo wa Mungu, ee,

Ee Mwana. ‘tuhurumie. x2


Mwana kondoo wa Mungu, ee , utujalie

Mwenye kuondoa dhambi zetu, ee


Amani utujalie, utujalie amani, ee

Amani utujalie, utujalie, ee,

Amani utujalie.

63 views0 comments

コメント

5つ星のうち0と評価されています。
まだ評価がありません

評価を追加
bottom of page