top of page

Cathedral Mass (Mwanampepo)



BWANA UTUHURUMIE


Ee Bwana Bwana utuhurumie – Ee Bwana Utuhurumie, ee Bwana utuhurumie

Ee Kristu ee Kristu utuhurumie – Ee Kristu utuhurumie ee Kristu utuhurumie

Ee Bwana Bwana utuhurumie – Ee Bwana Utuhurumie, ee Bwana utuhurumie


UTUKUFU


KIITIKIO: Utukufu kwa Mungu A/B: Utukufu

Kwa Mungu juu, kwa Mungu juu

Na amani duniani (kwa watu, watu wenye mapenzi mema ) x 2

1. Tunakusifu tunakuheshimu, tunakuabudu, tunakutukuza, tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu.

2. Ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni Mungu Baba mwenyezi, Ee Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee

3. Ee mwenye Bwana Mungu Mwanakondoo wa Mungu Mwana wa Baba.

4. Mwenye kuziondoa dhambi za dunia pokea ombi letu,

5. Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie.

6. Ndiwe uliye peke yako Mtakatifu peke yako mkuu Yesu Kristu,

7. Pamoja na Roho Mtakatifu katika utukufu wa Mungu Baba Amina.


NASADIKI


1. Tenor: Nasadiki kwa Mungu mmoja

KIITIKIO: Baba Mwenyezi Muumba Mbingu na nchi na vitu vyote

(Vinavyo-onekana na visivyo-onekana na visivyoonekana) x 2


2. Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu, Mwana wa pekee wa Mungu- Nasadiki kwa Mungu mmoja

3. Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote, Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli- Nasadiki kwa Mungu mmoja

4. Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba, ambaye vitu vyote vimeumbwa naye, ameshuka, mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu, na kwa ajili ya wokovu wetu - Nasadiki kwa Mungu mmoja

5. Akapata mwili kwa uwezo waroho mtakatifu, kwake yeye Bikira Maria akawa mwanadamu, akasulubiwa pia kwa ajili yetu akateswa kwa mamlaka ya ponsyo pilato akazaliwa.


Bass: Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa

Wote: (Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa) x 2

Bass: Akapaa mbinguni amekaa kuume kwa Baba

Wote: Atakuja tena kwa utukufu (kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake ni ufalme usio na mwisho) x 2

6. Nasadiki kwa Roho mtakatifu, Bwana na mleta uzima, atokaye kwa Baba na Mwana, anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na mwana, aliyenena kwa vinywa vya manabii- Nasadiki kwa Mungu mmoja

7. Nasadiki kwa kanisa moja Takatifu katoliki la mitume, naungama ubatizo mmoja, kwa maondoleo ya dhambi na ufufuko wa wafu, na uzima wa milele ijayo amina- Nasadiki kwa Mungu mmoja


MTAKATIFU


S/A: Mtakatifu, Bwana mtakatifu, Bwana mtakatifu Bwana Mungu

T/B: Mtakatifu Bwana Wote: Bwana Mungu wa majeshi

Sop: Mbingu na dunia Wote: Zimejaa utukufu wako mkuu

Hossana, Hossan juu mbinguni x 3

Sop: Mbarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana


MWANAKONDOO

SOP: Mwanakondoo wa Mungu Wote: Uondoaye dhambi utuhurumie x 2

BASS: Mwanakondoo wa Mungu Wote: Uondoaye dhambi za dunia x 2

Utupe amani, utupe amani.


3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page