top of page

Beba Mikononi


  1. Tusimame ndugu twende kwake Bwana (kweli) Usisite ndugu amka twende hima

  2. Peleka kwa moyo, moyo wa mapendo (kweli) Peleka kwa Bwana uliyojaliwa

  3. Sadaka ya fedha, fedha za mifuko (ndugu) Amka upeleke mezani kwa Bwana

  4. Mavuno mifugo, ni mali ya Bwana (kweli) Tupeleke kwake atazipokea

  5. Mkate divai tupeleke kwake (leo) Tupate baraka mbele zake Bwana

  6. Twende ndugu twende, mbele zake Bwana (twende) Tupeleke nafsi zetu kwake Bwana

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page