top of page

Banana/ Matoke Mass


1. Utukufu kwa Mungu juu mbinguni,na amani iwe kote duniani, kwa watu wenye mapenzi mema.

(Tunakusifu, Tunakuheshimu (na) Tunakuabudu Baba Tunakutukuza).

2. Tunakushukuru Mungu kwa ajili,Ya utukufu wako mkuu ee Bwana, ni Mungu ndiwe Mfalme wa mbinguni.

3. Ee Baba Mwenyezi, Bwana Yesu Kristu,Ee Mwana wa pekee ewe Mungu Mwana, ni Mungu ndiwe Mfalme wa mbinguni.

4. Mwenyezi kuziondoa dhambi za dunia, Utuhurumie tuhurumie, upokee Bwana maombi yetu.

5. Ndiwe mwenye kuketi kuume wa Baba, Utuhurumie kwa kuwa ndiwe, Pekee yako ni mtakatifu.

6. Pekee yako Bwana ndiwe mkuu, Ewe Yesu Kristu pamoja naye, Roho Mtakatifu milele yote.

88 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page