top of page

Bahati Bahati

Hii ndiyo siri ya maisha mema,

na tena utamu wa kumjua Yesu

Bahati kaacha karamu kubwa


(Bahati bahati nayo imwangukie nani Bahati

bahati aliyeipata ni nani imeandaliwa kwa

wote wenye moyo safi. Simama uonje na!

moyo wako utasisimka ) x2


Wateule mbona mnasitasita,

Hana ubaguzi wote awaita

Bahati kaacha karamu kubwa


Kama una dhambi nenda ukatubu,

Bwana hakatai mtu atubupo

Bahati kaacha karamu kubwa


Kama u mgonjwa, Bwana anaponya,

Kama una njaa utapata shibe

Bahati kaacha karamu kubwa


Yote ya dunia yakikukabili,

Piga moyo konde, nenda kwake Bwana

Bahati Kaacha karamu kubwa.

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page