top of page

Baba Mikononi Mwako

Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu x2.


1. Nimekukimbilia wewe, Bwana.nisiabike milele..

2. Kwa haki yako uniponye.Ee Bwana, Mungu wangu.

3. Mikononi mwako naiweka roho yangu, umenikomboa, ee Bwana, Mungu wa kweli.

4. Kwa sababu yu watesi wangu nimekuwa laumu naam, hasa kwa jirani zangu.

5. Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu,walioniona njiani walinikimbia.

6. Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa, nimekuwa kama chombo kilichovunjika.

7. Maana nimesikia masingizio ya wengi, hofu ziko pande zote.

8. Lakini mimi nakutumainia.Nimesema, wewe ndiwe Mungu wangu.

9. Nyakati zangu zimo mikononi mwako, uniponye na adui zangu,nao wanaonifuatia.

10. Umwangaze mtumishi wako kwa nuru ya uso wako, uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.

11. Iweni hodari, mpige moyo konde, ninyi nyote mnaomngoja Bwana.

5 views0 comments

Commentaires

Noté 0 étoile sur 5.
Pas encore de note

Ajouter une note
bottom of page