top of page

Azinta Mass


BWANA UTUHURUMIE.

Ee Bwana ‘tuhurumie – Ee Bwana

tuhurumie – (ee Bwana utuhurumie x2) x2.

Ee Kristu ‘tuhurumie - …

Ee Bwana…


UTUKUFU.

Utukufu kwa Mungu mbinguni, na amani kote duniani x2 / x1 / x2.

Tunakusifu, tunakuheshimu, twakuabudu, na kukutukuza.

  1. Twakushukuru mwenye utukufu, mfalme wa mbinguni Baba Mungu wetu.

  2. Ee Bwana Yesu Mwana wa pekee, ulie Mwana Kondoo wa Mungu.

  3. Mwenye kufuta dhambi za dunia ‘tuhurumie, utusikilize.

  4. Unaeketi kuume kwa Baba upeke yako ee Yesu Kristu.

  5. Pamoja naye, Roho Mtakatifu kwako, utukufu kwako Mungu Baba.

NASADIKI.

Ninasadiki kwa Mungu Baba x2 ninasadiki ninasadiki.

Ninasadiki kwa Mungu Baba, muumba mbinguni pia dunia: kwa Yesu Kristu, ninasadiki Mwana wa pekee wa Mungu Baba.

  1. Kapata mwili sawa na sisi kwa Roho wake Mtakatifu, akazaliwa naye Bikira, kateswa pia kasulubiwa.

  2. Kwa ajili yetu yeye kateswa; akafa kweli na akazikwa, akafufuka kwa wafu, kapaa mbinguni kwake Mwenyezi.

  3. Atarudi kwa utukufu, kuwahukumu wazima na wafu; ninasadiki kwa kanisa mmoja la kikatoliki pia la kitume.

  4. Nina ungama ubatizo mmoja, na ushirika wa utakatifu; maondoleo ya dhambi zetu ninangojea kufufuka ‘fufuko wa wafu.

  5. Uzima wote amina amina, milele yote amina amina.

MTAKATIFU.

(Mtakatifu x2 Bwana Mungu wa majeshi x2)

Mbingu zote na dunia zime jaa, utukufu

Wako. Hosanna x3. juu mbinguni x2

  1. (Mbarikiwa ajaye, jina lake Bwana Mungu x2)a

BABA YETU.

Alt:- Baba yetu mwema: BASS – uliye mbinguni, jina lako Baba na litukuzwe x2 ufalme wako (B/T:- Baba) utufikie (T/B Baba) utakalo Baba ( B/T:-Baba) na lifanyike. (Baba yetu mwema… x 2).

  1. Duniani Baba kama mbinguni, jina lako Baba nalitukuzwe.

  2. Tupe leo mkate wa kila siku, tusamehe Baba makosa yetu.

  3. kama tufanyavyo kwa ndugu zetu, jina lako Baba nalitukuzwe.

  4. ‘Situtie Baba kishawishini, bali maovuni utuopoe.

  5. kwa kuwa ‘falme na utukufu vyote Baba hata milele.

MWANAKONDOO.


(S: Mwana Kondoo wa Mungu. A/T:- Uondoaye dhambi. B;- za dunia. All:- Utuhurumie tunakuomba x 2). Tuhurumie. (S/A:- Mwana kondoo wa Mungu. All:- Unaye ondoa dhambi zetu utuhurumie tunakuomba x 2). S-A-T-B: - Mwana kondoo wa Mungu… (B:- Amani amani) utujalie amani tupe amani (B:- tupe [amani x 7]).

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page