top of page

Asiregee Moyowe

  1. Asiregee moyowe, asitoke machozi Akikumbuka Mungu wake, kwa yake makombozi, mtoa roho msalabani, mtaka kufa mwenyewe, kwa sababu kumpendani, nani mfunga moyowe.

  2. Bustani mle Getsemani, amwona Mungu Baba, je mtu Mungu ana nini, nguvu zake ni haba, Bwana wangu waziona, dhambi za binadamu mwili wako umetona, kama jasho la damu.

  3. Salamu Rabi salamu, anena Yuda mbaya, mwenye moyo wake mgumu, ambusu pasi haya aliwaambia basi, ntakayembusu ndiye, mtwaeni na kwa upesi, Yuda nani ni siye.

  4. Yuda nani sio yeye, aliyetenda dhambi, Tukimkosa Mungu Baba, kumdharau naye mwana, tukimsikitisha Roho, tu vipofu kama Yuda, tunatupa neema yake, itokayo kwake Yesu.

  5. Wote ni kupiga mbio, mitumewe pamoja, Wamtia mikono yao, askari walokuja Wampeleka hukumuni, aamuriwe na mtu Atokaye uwinguni, mwanzi mkuu wa watu.

  6. Mtume Petri amkanusha, amenena simjui Uhodari umekwisha, machoye hainui Pilato amwona Bwana, hakukosa ta neno Asema sioni dhambi, lakini ni mwoga mno.

  7. Hathubutu kumwachia, sioni nanawa mikono, mkimtaka Yesu muueni, la mwanzi hilo neno mara askari wamwanza, ni kupiga kelele, kumcheka na kumchokoza, mwenye mema milele

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page