top of page

Asiregee Moyowe



  1. Asiregee e moyowe, asitoke machozi, akimkumbuka Munguwe kwa yake makombozi, mtoa roho msalabani, mtaka kufa mwenyewe, kwa sababu kumpendani, nani mfunga moyowe.

  2. Bustani mle Getsemani amwoba Mungu Baba,je Mtu Mungu ananini, nguvu zake ni haba. Rabi yangu waziona, dhambi za binadamu, mwili wako umetona, kama jasho la damu.

  3. Salamu Rabi salamu, anena Yuda mbaya, mwenye moyo wake mgumu, ambusu basi haya. Aliwaambia basi, ntakaye mbusu ndiye, mtwaeni na kwa upesi, Yuda nani ni siye.

  4. Yuda nani ila yeye aliyetenda dhambi, akikosa kwa Munguwe, mtenda kwa dhambi yeye, mwenye kumtendea mema, mtaka dhambi haoni, kwamba ni kutupa neema, kumwendea shetani.

  5. Wote ni kupiga mbio mitumewe pamoja, namtia mikono yao, askari walokuja.

  6. Wampeleka hukumuni, ainuliwe na mtu, naye kutoka uwinguni, mwanzi mkuu wa watu.

  7. Mtume Petro amkanusha, amenena simjui, uhodari umekwisha, machoye hainui, Pilato amwona Rabi, hakukosa ta neno, asema sioni dhambi, lakini ni mwoga mno.

  8. Hadhubutu kumwachia, si hukumu aomba, mmoja nitamfungulia, Yesu au Baraba, mayahudi mwatakani? Baraba aachwe tu! Yesu afe msalabani, damuye juu yetu.

  9. Pilato hukumu gani, simo nanawa mkono, mkitaka Yesu mueni, la mwanzi lilo neno, mara askari mwamwanza, ni kumpiga kelele, kumcheka na kumchokoza, mwenye mema milele.

  10. Wamfunga mikono nyuma wapiga fimbo mia, hata mwili wake mzima, madonda kuenea, si mwisho wa makutano, ana miiba kichwani, na mwanzi katika mkono, huamkiwa “Sultani.”

  11. Nguvu zake zimekwisha, na damu kumtokea, kwanza ya kumsulubisha, mumpe ajaporegea, wampachika mabegani msalaba wa mti mzito, wamsukumiza njiani, njia ya makokoto.

  12. Wakifika Kalvarini, mavazi wamvulia, misumari msalabani, kwa nyundo wampigia, kati ya wevi wawili, wamsimamisha Mwokozi, naye ni Mtu Mungu kweli, taa letu kombozi.

  13. Ndungu zangu mwangalieni, Mkombozi mwenye mema, akifungwa msalabani, usoni kwake mama, sikieni mapendoye, mjute yenu makosa, mjipatie rehemaye, kwamba wakati sasa!

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page