top of page

Asante Mungu


  1. Ehee nakumbuka kule nilikotoka; Ahaa najiuliza mimi nisemeje Ehee kigugumizi kinanikamata; Ahaa najiuliza mimi najihoji tu Sina neno mimi sina jipya la kusema, umetenda wema mpaka unanishangaza. Nashukuru Bwana asante Mungu tena sana asante, asante Mungu sina maneno asante asante Mungu

  2. Ehee ulinigusa tumboni mwa mama; Ahaa... Ehee nikazaliwa tayari kwa kazi; Ahaa...

  3. Ehee ukanipa kuwainua watu; Ahaa... Ehee wakakuimbia na kukusifu; Ahaa...

  4. Ehee dunia iliponishambulia; Ahaa... Ehee ukasimama ukanitetea; Ahaa...

  5. Ehee nitakuimbia na nyumba yangu; Ahaa... Ehee tutakusifu siku za uhai; Ahaa...


Hitimisho

Ama kweli iya unanishangaza wewe ni mwema, Ama kweli iya unapenda watu wewe ni mwema, Ama kweli iya unawathamini wewe ni mwema, Nashukuru hiya Nashukuru sana wewe ni mwema Nakusifu hiya nakusifu sana wewe ni mwema Siku zote hiya nitakuimbia wewe ni mwema we ni mwema wewe ni mwema (ni mwema) wewe ni mwema na mpole wewe ni mwema ni mwema wewe ni mwema ni mwema Hiya



4 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page