top of page

Asante Mama wa Yesu


Asante Mama wa Yesu, asante sana Mama Maria Uliye muombezi wetu, sisi wanao wa dunia Baraka za mwana wako, tunazipata kweli Maria Yote ni kwa ajili yako, muombezi mwema Maria

  1. Faraja tunazipata, udhaifu unatoweka Unyonge unatutoka, imani inaongezeka

  2. Walemavu na wagonjwa, Yesu awafariji sana Na pia anawaponya, na kuwaongezea neema

  3. Mapepo wote wabaya, na yule shetani muovu Haraka wanakimbia, kwa jina la mwanao Yesu

  4. Uzidi kutuombea, tupate nguvu na uzima Tusije tukapotea, tufike mbinguni kwa Baba

5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page