top of page

Asante kwa Mema


Nakushukuru ee Bwana muumba wa vyote; Asante kwa mema yote uliyonijalia x 2

  1. Umenilinda vyema, katika maisha, ukanijalia na afya njema mwilini. Umenilinda vyema, katika safari, ukaniepusha na ajali za njiani.

  2. Ukanipa chakula, cha uzima wangu, chakula bora kitiacho nguvu mwilini. Ukanipa kinywaji, cha uzima wangu, kinywaji bora kitiacho nguvu mwilini.

  3. Ukanilinda Bwana, na maovu mengi, ukanipa ukamilifu nikukumbuke. Ukanikinga Bwana, na pepo wachafu, ukanitaka nitangaze ukuu wako.

  4. Hakika wanipenda, na unanijali, tangu utoto wangu wala hukunitupa. Mimi ni kitu gani, hata unijali, thamani yangu kweli si kitu mbele yako.

  5. Ee Mungu wangu mimi, nakupenda sana, fadhili zako Bwana kwangu ninaziona. Maisha yangu yote, ninakuwachia, ili moyo wangu ushibe upendo wako.

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page