top of page

Amkeni Kyenzenzelu


Amkeni watu wa mataifa yote chenzenzelu tumsifu Mungu wetu mwenye uwezo chenzenzelu

Kwa maana Bwana Mungu ametenda mambo makuu ya ajabu chenzenzelu (tuimbe tucheze tumsifu Mungu wetu chenzenzelu) x2


Simameni wazee kwa vijana wote kwa furaha tumsifu,

(Tumwimbie Jalali wetu Mwenyezi Mtawala) X2


Ni Mfalme, bendera ya wokovu wetu kwa furaha tumsifu,

(Tumpe sifa kiongozi wetu Shupavu Mtawala) X2


Kwa hakika ni Alfa na ndiye Omega kwa furaha tumsifu,

(Jemedali hoye hoye ni Mshindi Mtawala) X2


Tumwimbie dunia nayo itetemeke kwa furaha tumsifu,

(Tuchezee milima nayo iyumbe mtawala) X2


Tumuhimidi aliyeumba vitu vyote kwa furaha tumsifu,

(Bahari ya duniani na Mbinguni Mtawala) X2

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page