top of page

Amini Kweli

1. Amini kweli nawaambieni mwanitafuta, Ni kwa sababu mlikula ule mkate, si kwa sababu mliziona zile ishara, bali sababu mlikula mkashiba, bali sababu mlikula mkashiba

Amini amini nawaambieni kuna chakula kinachowafaa, nacho chakula ndicho kile cha uzima wa milele.

2. Msikitendee kazi chakula kinachopita bali chakula kidumucho na milele, chakula Musa alichowapa hakiwafai, kweli Babangu anawapa kiwafaacho, kweli Babangu anawapa kiwafaacho..

3. Kile chakula chenye uzima kweli ni mimi, ajaye kwangu hataona njaa kamwe, anayekula huu mwili wangu, na kuinywa damu, hukaa kwangu nami hukaa ndani yake,hukaa kwangu nami hukaa ndani yake..

4. Hicho chakula chenye uzima kweli ni mimi, kilicho shuka toka mbinguni kwa Baba, mtu akila chakula hiki hatafariki, bali anao ule ‘zima wa milele, bali anao ule ‘zima wa milele..

5. Kile chakula ninachotoa ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu, msipoula huu mwili wake Mwana Adamu, na kuinywa damu hamna ‘zima ndani yenu, na kuinywa damu, hamna ‘zima ndani yenu

6. Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu, ana uzima nami nitamfufua. Na mwili wangu ndichi chakula kile cha kweli, na damu yangu ndicho kinywaji cha kweli, na damu yangu, ndicho kinywaji cha kweli……

7. Na kama Baba alye hai alivyonituma, nami ni hai, ndimi ni hai kwa Babangu, na kadhalika mwenye kunila ana uhai, kweli nasema atakuwa hai, kwangu, kweli nasema, atakuwa hai kwangu….

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page