top of page

Amezaliwa Masiha Wetu

Amezaliwa Masiha wetu, hoyee hoye hoye Mwana wa Mungu mkombozi wetu, hoyee hoye hoye Leo kazaliwa naye Maria na amelazwa kwenye hori la wanyama, twende tukamwone Amekuja kwetu mwana wa Mungu kuzichukua dhambi zetu wanadamu, mkombozi wetu { Tumsujudie Bwana Mungu, kwa vigelegele Tucheze ngoma na kayamba tupige makofi } *2


Amelala manyasini, twendeni tukamwone, tukamsalimie Mkombozi wetu kwa zawadi zetu za dhahabu uvumba na manemane


Wachungaji waondoka, waenda Bethlehemu, Wakamsujudie Bwana Mkombozi, wafurahi naye pamoja na Maria naye Yusufu


Malaika wamefika wengi na wa mbinguni tukajiunge nao tuimbe pamoja utukufu uwe kwa Mungu juu amani kwa watu wenye mapenzi mema


Tumpokee mkombozi Masiha amekuja ewe mtoto Yesu ishi ndani yetu, tuangaze sisi, kwa mwanga wako mwanga wa Mbinguni.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page