top of page

Amacea Mass


[s/a] Bwana Utuhurumie, (ee Bwana)

[w] Bwana utuhurumie x2


[t/b] Kristu utuhurumie, (ee Kristu)

[w] Kristu utuhurumie x2


Bwana ….


UTUKUFU

1. Utukufu kwa Mungu juu mbinguni Na amani kote duniani (Kwa watu) wenye mapenzi mema Tunakusifu Baba, tunakuheshimu, Twakuabudu sisi tunakutukuza  2. Twakushukuru Mungu kwa ‘tukufu Wako mkuu ewe Mungu mfalme (Ee Baba) wa Mbingu Baba yetu

3. Bwana wetu mwokozi Yesu Kristu Mwana wa pekee wake Mungu (Uliye) Mwanakondoo wa Mungu

4. Unayeziondoa dhambi zote Za dunia utuhurumie (Pokea) pokea ombi letu

5. Wewe unayeketi kuume Kwake Baba utuhurumie (Sikia) sikia ombi letu

6. Kwani pekee yako ndiwe Bwana Pekee yako mkuu na mkombozi (Pekee) pekee Yesu Kristu

7.  Kwa umoja wa Roho mtakatifu Ndani yake Baba watukuzwa (Ee Yesu) milele na milele


NASADIKI

Nasadiki kwa Mungu mmoja - Mimi nasadiki

Ndiye Baba yetu Mwenyezi “

Muumba mbingu pia dunia. “

Nasadiki kwa Yesu Kristu. “

Ninasadiki x2, mimi nasadiki (nasadiki ninasadiki) mimi nasadiki x2


Mwana wa pekee wa Mungu – Mimi nasadiki

Aliyezaliwa kwa Baba– Mimi nasadiki

Akapata mwili kwa Roh– Mimi nasadiki

Kazaliwa naye Bikira– Mimi nasadiki


Kisha yeye kasulibiwa – Mimi nasadiki

Kwa mamlaka yake Pilato– Mimi nasadiki

Kwa ajili yetu Kateswa – Mimi nasadiki

Alikufa na akazikwa– Mimi nasadiki

Kafufuka katika wafu – Mimi nasadiki

Akapaa juu mbinguni – Mimi nasadiki

Ameketi kuume kwake – Mimi nasadiki

Mungu Baba yetu Mwenyezi– Mimi nasadiki


Ndipo atakapotokea – Mimi nasadiki

Kuwa hukumu wote – Mimi nasadiki

Kwake Roho Mtakatifu– Mimi nasadiki

Kwa kanisa la Katoliki– Mimi nasadiki


Ushirika wa watakatifu – Mimi nasadiki

Ondoleo la dhambi zetu– Mimi nasadiki

Nangojea ‘fufuko wa miili – Mimi nasadiki

Na uzima wa milele– Mimi nasadiki


MTAKATIFU

Tenor: Mtakatifu, mtakatifu Bwana All: Mungu wa majeshi Sop: Mtakatifu Bwana All: Mungu wa majeshi S/A Mbingu na dunia zimejaa, zimejaa All: Mbingu na dunia , zimejaa utukufu wako S/A Mbingu na dunia All: Zimeja utukufu wako.

Hosana juu x4 mbinguni.

Mbarikiwa ‘naye kuja, mabrikiwa ‘naye kuja, mbarikiwa. Mbarikiwa ‘naye kuja kwa jina, jina lake Bwana.


FUMBO LA IMANI

Yesu Kristu alikufa, Yesu Kristu kafufuka, Yesu Kristu atakuja, atakuja kwetu tena.


BABA YETU

Baba yetu Baba wa mbinguni, jina lako Baba litukuzwe, Ufalme wako Baba na ufike, utakalo Baba lifanyike

Duniani kama mbinguni Ee Baba – Utakalo lifanyike

Tupe leo riziki zetu ee Baba – Utakalo lifanyike

Riziki zetu za kila siku Ee Baba – Utakalo lifanyike


Dhambi zetu utusamehe Ee Baba – Utakalo lifanyike

Kama vile twasamehe Ee Baba – Utakalo lifanyike

Waliotukosea sisi Ee Baba – Utakalo lifanyike


‘Situtie kishawishini Ee Baba – Utakalo lifanyike

Walakini utuopoe Ee Baba – Utakalo lifanyike

Maovuni utuopoe Ee Baba – Utakalo lifanyike


Kwa kuwa ufalme ni wako Ee Baba – Utakalo lifanyike

Nayo nguvu, na utukufu Ee Baba – Utakalo lifanyike

Daima daima milele Ee Baba – Utakalo lifanyike


AMINA

S/A Amina, Amina, All: Amina, Amina, Amina, Amina, x2


MWANA KONDOO

Tenor: Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, All: Ee Mwana utuhurumie Sop: Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia All: Ee Mwana utuhurumie. Bass Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia All: Ee Mwana, utujalie amani

10 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page