top of page

Akamba Mass



BWANA TUHURUMIE

Ee Bwana tuhurumie, ee Bwana ee,

Bwana tuhurumie


Kristu tuhurumie

Ee Kristu tuhurumie x3


UTUKUFU

Utukufu juu kwa Mungu mbinguni

Na amani duniani kwa watu wa mapenzi

wenye mapenzi mema. Tunakusifu (Baba) tunakuheshimu.

Tunakuabudu (Baba) tunakutukuza.


Baba tunakushukuru kwa ajili ya utukufu,

utukufu wako mkuu.


Ewe Mungu ni mfalme wa Mbinguni,

Mungu Baba, Baba ndiwe Mwenyezi.


Ewe Bwana Yesu Kristu ndiwe mwana

wake Mungu, ndiwe mwana wake Baba.


Ewe Bwana Mungu Mwana kondoo wake

Mungu, Mwana wake Baba


Ewe mwenye kuondoa zetu dhambi za

dunia, Bwana utuhurumie.


Ewe mwenye kuketi kuume kwake Baba,

ewe utuhurumie.


Ni kwa kuwa ndiwe uliye pekee yako

Mtakatifu, Bwana Yesu Kristu.


Na pamoja naye Roho Mtakatifu katika

utukufu wa Mungu Baba.


NASADIKI

Nasadiki kwa Mungu mmoja.

Nasadiki kwa Mungu mmoja

Muumba mbingu na dunia na kwa Yesu Kristu

mwanaye wa pekee Bwana wetu,

Nasadiki ninasadiki (mimi) kweli ninasadiki,

nasadiki kwa Mungu mmoja.


Alipata mwili kwa tendo lake Roho Mtakatifu, kazaliwa naye Bikira, akateswa kwa ponsio pilato.


Akasulibiwa akafa, akazikwa kaburini, na kuzimu akashukia,

kafufuka siku ya tatu.


Akapaa juu mbinguni, ameketi kuume kwa Baba, Mungu Baba yetu mwenyezi Muumba mbingu na dunia.


Ndipo atakapotokea kuhukumu wazima na wafu, na ufalme wake milele utakuwa bila mwisho.


Nasadiki kanisa ni moja, ni kanisa takatifu,

ni kanisa la katoliki ni kanisa la mitume.


Ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi zetu, nasadiki ufufuko wa miili, na uzima wa milele.


HALLELUYA

Halleluyaia

Halleluia, alleluia (halleluia)

Halleluia halleluia x2


AMINA

Amina

Amina, amina (amina)

Amina, amina x2


MTAKATIFU

Mtakatifu Bwana

Mtakatifu Bwana, Mtakatifu Bwana

(Bwana) Mungu wa majeshi x2

Mbinguni na dunia zimejaa utukufu wako

hosanna juu mbinguni,

hosanna (hosanna) juu mbinguni.

Mbarikiwa ajaye kwa jina lake Bwana

Hosanna juu mbinguni,

hosanna (hosanna) hosanna juu mbinguni x2


BABA YETU

Baba yetu

Uliye juu mbinguni jina lako litukuzwe,

(Ee Baba)


Ufalmeo ufike utakalo lifanyike duniani

kama Mbinguni. Baba wa mbinguni jina

lako litukuzwe.


Utupe leo mkate, mkate wetu na utupe

tupe mkate wa kila siku. Baba wa

mbinguni jina lako litukuzwe.


Makosa tusamehe kama vile twasamehe

watu waliotukosea. Baba wa mbinguni

jina lako litukuzwe.


Usitutie penye kishawishi walakini

maovuni utuopoe. Baba wa mbinguni

jina lako litukuzwe.


Kwa kuwa ufal me ni wako na nguvu na

utukufu hata milele. Baba wa mbinguni

jina lako litukuzwe.


MWANAKONDOO

Mwanakondoo Mwana wa Mungu uondoaye dhambi za

dunia utuhurumie x2

Mwanakondoo, Mwana wa Mungu uondoaye dhambi za

dunia. Utuhurumie. Utujalie, utujalie, amani Utujalie, utujalie, utujalie amani. X3


5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page