BADA YA MWANZO
P: Kwa jina la Baba na la Mwana na la
Roho Mtakatifu
W: Amina
P: Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na
upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa
Roho Mtakatifu viwe nanyi nyote
W: Na viwe rohoni mwako
AU
P:Neema na amani, kutoka kwa Mungu,
Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo,
viwe nanyi.
W: Na viwe rohoni mwako
AU
P: Bwana awe nanyi
W: Na awe rohoni mwako
P: Ndugu zangu, tukiri dhambi zetu, ili
tupate kustahili kuadhimisha mafumbo
matakatifu
W: Namwungamia Mungu Mwenyezi,
nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa
mno kwa mawazo, kwa matendo, na
kwa kutotimiza wajibu: nimekosa mimi,
nimekosa mimi, nimekosa mno. Ndiyo
maana namwomba Maria mwenye heri,
Bikira daima, Malaika na Watakatifu
wote, nanyi, ndugu zangu, niombeeni kwa
Bwana Mungu wetu.
W: Amina
AU
P: Ee Bwana, utuhurumie
W: Kwa kuwa tumekukosea
P: Ee Bwana, utuonyeshe huruma yako
W: Utupe na wokovu wako
P: Mungu Mwenyezi atuhurumie na,
atusamehe dhambi zetu, atufikishe
kwenye uzima wa milele
W: Amina
AU
P: Ndugu zangu, tukiri dhambi zetu, ili
tupate kustahili kuadhimisha mafumbo
matakatifu.
P: Wewe uliyetumwa kuwaponya wenye
moyo wa toba, Bwana, utuhurumie
W: Bwana, utuhurumie au Kyrie, eleison
P: Wewe uliyekuja kuwaita wakosefu,
Kristo, utuhurumie
W: Kristo, utuhurumie au Christe, eleison
P: Wewe uketiye kuume kwa Mungu
160
YAL OO
Baba, ukituombea, Bwana, utuhurumie
W: Bwana, utuhurumie au Kyrie, eleison
P: Mungu Mwenyezi atuhurumie na,
atusamehe dhambi zetu, atufikishe
kwenye uzima wa milele
W: Amina
UTUKUFU
Kila inapoagizwa, utenzi unaimbwa, au
unasemwa
Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Na amani duniani / kwa watu wenye
mapenzi mema.
Tunakisifu / tunakuheshimu.
Tunakuabudu / tunakutukuza.
Tunakushukuru / kwa ajili ya utukufu
wako mkuu.
Ee Bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni,
Mungu Baba Mwenyezi.
Ee bwana Yesu Kristu / Mwana Wa pekee
Ee Bwana Mungu, Mwana kondoo wa
Mungu, Mwana wa Baba.
Mwenye kuondoa dhambi za dunia, /
utuhurumie.
Ewe mwenye kundoa dhambi za dunia,
Pokea ombi letu.
Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba, /
utuhurimie.
Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako
Mtakatifu, peke yako Bwana, / peke
yako Mkuu / Yesu Kristu.
Pamoja na Roho Mtakatifu,
Katika Utukufu wa Mungu Baba. Amina
SALA
Kuhani, hali amefumba mikono, anasema:
Tuombe.
Wote wanakaa kimya kidogo wakisali ,
hapo kuhani anafumbua mikono, na kusema
sala ya kolekta
Mwisho
W. Amina.
LITURUJIA YA NENO
SOMO LA KWANZA
Wote huketi
Mwisho: neno la Bwana.
W. Tumshukuru Mungu.
WIMBO
SOMO LA INJILI
Ee Mungu Mwenyezi,
Utakase moyo wangu na midomo yangu,
Niweze kutangaza vema Injili yako
takatifu.
Wote husimama.
Bwana awe nanyi.
W. na awe rohoni mwako.
Somo katika Injili ilivyoandikwa na…
W. Utukufu kwako, ee Bwana.
Fanya ishara ya msalaba kwa kidole gumba
juu ya kitabu, usoni,midomoni na kifuani.
Mwisho: neno la Bwana.
W. sifa kwako, ee kristu.
Padre anabusu Injili akisema;
Dhambi zetu ziondolewe kwa Injili
iliyosomwa
NASADIKI
Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi
Muumba mbingu na nchi, na vitu vyote
vinavyoonekana, na visivyoonekana.
Nasadiki kwa Bwana mmoja yesu Kristu,
Mwana wa pekee wa Mungu. Aliyezaliwa
kwa Baba tangu milele yote.
161
ALL GLORY TO JESUS
Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga
kwa mwanga,
Mungu kweli kwa Mungu kweli.
Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye
Umungu mmoja na Baba, ambaye vitu
vyote vimeumbwa naye.
Ameshuka toka mbinguni kwa ajili yetu
sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu
wetu.
Akapata mwili kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria
akawa Mwanadamu. Akasulibiwa pia
kwa ajili yetu sisi, akateswa kwa mamlaka
ya Ponsyo Pilato, akafa, akazikwa.
Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
Akapaa mbiguni amekaa kuume
kwa Baba atakuja tena kwa utukufu
kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme
wake hautakuwa na mwisho.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu Bwana
mleta uzima atokaye kwa Baba na
Mwana anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na Baba na Mwana aliyenena
kwa vinywa vya Manabii.
Nasadiki kwa kanisa moja, takaifu
katoliki la Mitume Naungama ubatizo
mmoja kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu. Na uzima
wa milele ijayo. Amina.
SALA YA WAUMINI
Ndungu zangu, tumwombe Mungu Baba
Mwenyezi asikilize kwa wema sala zetu
Kwa ujumbe wa Yesu Kristu Bwana wetu.
Msomaji anaweza kutaja maombi mengine;
na mwisho Padre anasema:
Ee Mungu, uliye makimbilio na nguvu
yetu, uliye asili ya wema wote,
Usikilize sala za Kanisa lako,
Utujalie ili hayo tunayoomba kwa imani,
Tuyapate kweli.
W. Amina.
LITURUJIA YA EKARISTI
KUTAYARISHA DHABIHU
Padre anatolea mkate;
Utukuzwe, ee Bwana, Mungu wa
ulimwengu, maana kwa wema wako
tumepokea mkate huu tunaokutolea.
Mkate huu ni mazao ya nchi na kazi
ya mikono ya wanadamu. Utujalie uwe
kwetu mkate wa uzima na milele.
W. Atukuzwe Mungu milele
Padre anatia maji katika divai;
Kwa fumbo la maji haya na divai hii
tujaliwe kushiriki Umungu wa Kristu,
aliyekubali kushiriki ubinadamu wetu.
Padre anatolea divai;
Utukuzwe, ee Bwana, Mungu wa
ulimwengu, maana kwa wema wako
tumepokea divai hii tunayokutolea.
Divai hii ni tunda la mzabibu na kazi ya
mikono ya wanadamu. Utujalie iwe kwetu
kinywaji cha roho.
W. Atukuzwe Mungu milele
Ee Bwana, utupokee sisi tunaokunyenyekea
na kutubu moyoni; na hivyo sadaka
yetu ifanyike leo mbele yako, ili ipate
kukupendeza, ee Bwana Mungu.
Padre ananawa mikono:
Ee Bwana, unioshe kabisa na uovu wangu
unitakase dhambi zangu.
162
YAL OO
Padre anawaelekea waumini akiwambia:
Salini ndugu: Ili sadaka yangu na yenu
ikubaliwe na Mungu Baba Mwenyezi.
W. Bwana apokee sadaka mikononi
mwako kwa sifa na utukufu wa jina lake
na pia kwa manufa yetu sisi na mafaa ya
kanisa lake lote takatifu.
Sala ya kuombea dhabihu:
…daima na milele
W: Amina.
UTANGULIZI
Hapo kuhani anaanza sala ya Ekaristi. Hali
amefumbua mikono, anasema
Bwana awe nanyi
Na awe rohoni mwako
Inueni mioyo.
Tumeiinua kwa Bwana.
Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
Ni vema na haki
KAWAIDA I
Kweli ni vema na haki tukushukuru daima
na popote, ee Bwana, Baba Mwema,
Mungu Mwenyenzi wa milele, kwa njia ya
Kristu bwana wetu.
Ndani yake ulipenda kukamilisha vitu
vyote, ukatujalia sisi sote kushiriki utajiri
wake. Ingawa yeye alikuwa Mungu,
alijishusha mwenyewe, akaleta amani
duniani kwa damu yake msalambani.
kwa sababu hiyo ametukuzwa zaidi ya
vitu vyote, akawapatia wokovu wa milele
wote wanaomsadiki na kumfuata.
Kwa hiyo, sisi pamoja na majeshi yote ya
malaika wa mbinguni twaimba wimbo wa
utukufu wako, tukisema bila mwisho:
KAWAIDA II
Kweli ni vema na haki tukushukuru daima
na po pote, ee Bwana, Baba Mwema,
Mungu Mwenyenzi wa milele. Ulimwumba
mtu kwa wema wako, naye alipolaaniwa
kwa haki, ulimkomboa kwa huruma yako:
kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
majeshi yote ya malaika wa mbinguni
wanafurahi kutangaza utukufu wako,
Nasi twaungana nao tukisema kwa
unyenyekevu:
Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu Bwana
Mungu wa majeshi, Mbingu na dunia
zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.
(Watu wote wanapiga magoti)
SALA YA EKARISTI
Kuomba mageuzo ya mkate na divai
Kwa hiyo, ee Baba mwingi wa huruma,
tunakusihi kwa unyenyekevu na kukuomba
kwa njia ya Yesu Kristo, Mwanao, Bwana wetu
Anafumba mikono
Uvipokee na kuvibariki † vipaji hivi,
sadaka hizi, dhabihu hizi takatifu na safi,
Hali amefumbua mikono, anaendelea kusema:
Tunazokutolea kwanza kabisa kwa ajili
ya kanisa lako takatifu katoliki. Ukubali
kuliletea amani, kulilinda, kulikusanya
katika umoja na kuliongoza popote
duniani, pamoja na mtumishi wako Baba
Mtakatifu (F) na askofu wetu (F) na wote
wenye kushika imani ya kweli, katoliki na
ya Mitume.
163
ALL GLORY TO JESUS
Kwa hiyo, ee Bwana, tunakuomba upokee
kwa wema sadaka tunayokutolea sisi
watumishi wako, na familia yako yote. Na
uziweke siku zetu katika amani yako, na
uamuru tuopolewe na laana ya milele na
tuhesabiwe katika kundi la wateule wako.
Kwa njia ya Kristu Bwana Wetu. Amina
Ewe Mungu tunakuomba, uibariki sadaka
hii, ikupendeza, uipokee, iwe sadaka
yenye maana, na inayokubalika katika
yote: ili iwe kwetu Mwili na Damu ya
Mwanao Bwana wetu Yesu Kristu.
Siku iliyotangulia kuteswa kwake,
Anatwaa mkate, na kuuinua kidogo juu ya
altare yeye alitwaa mkate katika mikono
yake mitukufu, akainua macho mbinguni
kwako wewe Baba yake Mwenyezi,
akakushukuru na kukutukuza, akaumega,
akawapa wafuasi wake akisema:
Twaeni, mle wote;
Huu ndio mwili wangu,
Utakaotolewa kwa ajili yenu.
Vivyo hivyo baada ya kula,
Anatwaa kikombe, na kwa kukiinua
kidogo juu ya altare, anaendelea
kutamka
Akatwa kikombe katika mikono yake
mitukufu, akakushukuru na kukutukuza,
Akawapa wafuasi wake akisema.
Twaeni mnywe wote;
Hiki ni kikombe cha damu yangu,
Itakayomwagika kwa ajili yenu na kwa
ajili ya wote
Kwa maondoleo la dhambi. Fanyeni hivi
kwa kunikumbuka mimi.
Fumbo la imani:
W. Ee Bwana tunatangaza kifo chako
na kutukuza ufufuko wako mpaka
utakapokuja.
Kwa hiyo, ee Bwana, tunapokumbuka
kufa kwake mwanao, tunakutolea mkate
wa uzima na kikombe cha wokovu
Tunakushukuru kwa kuwa umetujalia
tusimame mbele yako na kukutumika.
Kuliombea kanisa:
Tunaomba kwa unyeyekevu, Roho
Mtakatifu atufanye tuwe jamaa moja sisi
tunaoshiriki Mwili na Damu ya kristu
Ee Bwana,
Ulikumbuke kanisa lako po pote duniani,
utukamilishe katika upendo, sisi pamoja
na Baba Mtakatifu wetu (F) na askofu
wetu (F) na watumishi wako wote.
Umkumbuke mtushi wako
Uliyemwita kwako
Kutoka dunia hii.
Kwa kuwa kwa Ubatizo, alishiriki kifo cha
Kristu, umjalie ashirki pia ufufuko wake.
Uwakumbuke pia ndugu zetu, waliofariki
wakiwa na tumaini la ufufuko.
Uwakumbuke na marehemu wote,
uwapokee kwenyu nuru ya uso wako.
Tunakuomba utuhurumie sisi sote, ili
tustahili kushiriki uzima wa milele na
kukusifu na kukutukuza pamoja na
Maria Bikira mwenye heri mama wa
Mungu, mitume wenye heri na watakatifu
wote walio kupendeza tangu kale.
Tunakuomba hayo kwa njia ya mwanao
Yesu Kristu.
Kwa njia yake, pamoja naye, na ndani
yake, wewe Mungu Baba Mwenyezi
katika umoja wa Roho Mtakatifu unapata
heshima na utukufu wote, daima na milele
W. Amina
Tazama Mwana Kondoo wa Mungu,
Tazama aondoaye dhambi za dunia.
Heri yao walioalikwa kwenye karamu ya
mwanakondoo.
Wote husema mara moja
Ee Bwana, sistahili uingie kwangu lakini
sema neno tu na roho yangu itapona.
Mwili wa Kristo unilinde nipate uzima wa
milele
Damu ya Kristo inilinde nipate uzima wa
milele.
IBADA YA KUMALIZIA
Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako
Awabariki Mungu Mwenyezi, Baba na
Mwana na Roho Mtakatifu.
W. amina
Nendeni na amani
W. Tumshukuru Mungu
PRAYER AFTER COMMUNION
ANIMA CHRISTI
Soul of Christ, sanctify me.
Body of Christ, save me.
Blood of Christ, run through my veins.
Water from the side of Christ, wash me.
Passion of Christ, strength me.
O good Jesus, hear me.
Within your wounds, hide me.
Let me not be separated from thee.
From the evil enemy, defend me.
At the hour of death, call me.
And bid me come to Thee.
That with your saints I may praise thee
For all eternity. Amen.
IBADA YA KOMUNYO
Na sasa tusali kwa imani ile sala
aliyotufundisha Bwana wetu
W. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako
litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo
lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
utusamehe makosa yetu, kama
tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi lakini utuopoe
maovuni.
Ee Bwana,
Tunakuomba utuopoe katika maovu
yote, utujalie kwa wema amani maishani
mwetu.
Utuepushe daima na dhambi kwa huruma
yako, tusifadhaishwe na jambo lo lote
Tungojee kwa matumaini kurudi kwake
mkombozi wetu Yesu Kristu.
W. kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu,
na utukufu hata milele
Ee Bwana Yesu Kristu, uliyewaambia
mitume wako; nawaachieni amani,
nawapeni amani yangu; usizitazame
dhambi zetu ila tu imani ya kanisa lako;
ulijalie amani na umoja kama yalivyo
mapenzi yako. Unayeishi na kutawala
daima na milele.
W. Amina.
Amani ya Bwana iwe daima nanyi
W. Iwe Pia Nawe
Tutakiane amani
W. Mwana kondoo wa Mungu,
Uondoaye dhambi za dunia / utuhurumie
Mwana kondoo wa Mungu,
Uondoaye dhambi za dunia / utuhurumie
Mwana kondoo wa Mungu,
uondoaye dhambi za dunia / utujalie
amani