UZIMA WETU UPO KATIKA KUMKIRI NA KUMSADIKI KRISTO
Nguvu ya kuushinda Ulimwengu yaani tamaa mbaya, maovu, mienendo batili ya ulimwengu huu ni kumwamini Kristo, mwana wa Mungu.Kwa kuwa na imani kwa Mungu tunapata auheni katika maisha yetu.Imani hiyo ndio yenye kutupatia uzima wa milele. Mtu mwenye ukoma alipomwona Yesu alianguka kifudifudi na kuomba kutakaswa. Yesu Kristo anamtakasa. Mkoma huyu amemwamini Yesu, ametambua nguvu yake ya kuponya, na kuponywa kwake kunamdumishia uzima.
Ndugu zangu , katika maisha yetu tuna aina mbalimbali za magonjwa, tunaumwa akili, tunaumwa viungo vya miili yetu, tunaumwa kwa kukosa huruma na upendo. Kuumwa huku kunatukosesha raha, kunatuondolea uzima. Njia pekee ya kupata tiba ni kutakaswa. Yeye ndiye mwenye kutuponya , mwenye kutupatia matibabu, kutupatia akili ya kupeana ushauri. Yeye ndiye mwenye kutuwezesha akili ya kugundua na kuvumbua vitu.
Sala
Ee Mwenyezi Mungu, tunakuomba utupe Neema za kuendelea kukukiri na kukuamini wewe,Amina
@ Claretian Publication