SHAUKU YA KUMWONA YESU HUJENGWA KATIKA IMANI
Leo tunakutana na watu wenye imani na walio na hamu ya kumwona Yesu. Eliyazari alisimama imara katika imani, na akakataa kupotoshwa kwa kufanya yaliyo haramu. Alisema, “Sitaweza kuepukana na mikono ya Mwenyezi Mungu nikiwa hai au nikiwa nimekufa.” Huu ni ujasiri mkuu wa kukubali kuwa Mungu ndiye mweza yote na haepukiki. Haifai kumridhisha mwanadamu huku unamuudhi Mungu. Zakayo naye katika Injili akitamani kumwona Yesu, aliisahau hadhi yake, heshima na utajiri, akaukwea mti. Hebu waza, wakati wa andamano la Ekaristi, ukimwona Waziri ameupanda mti ili amwone Yesu kwenye Ekarosti Takatifu. Inakuwaje sisi huona haya kumtangaza na kumkiri Yesu? Mbona wewe wataka kumweka Yesu pembeni, huna haja hata ya kwenda kanisani? Tujifunze kutoka kwa Zakayo. Tusione haya kumtangaza Kristo, tukiwaza watakayoyasema watu. Hili ni elezo tosha kuwa sharti tuzisake baraka kwa vyovyote vile.
_*Sala* Yesu mwema tujalie moyo wa unyenyekevu hasa tunapojaliwa uwezo au cheo katika maisha.*Amina*_
@Claretian Publication