KUMSADIKI NA KUMKIRI KRISTO NI KUURITHI UZIMA WA MILELE
Yohane Mbatizaji kwa unyenyekevu mkubwa, anakiri kuwa yeye siye Kristo, wala Eliya, wala Manabii. Anakiri kuwa yeye ni mtayarishaji tu wa njia ya Kristo.Anakiri kuwa Kristo atakuja,ambaye yeye Yohane hastahili hata kuilegeza gidamu ya kiatu chake. Yohane ni mfano bora wa watu wanaomkiri Kristo, anasadiki juu ya uwezo wa Kristo hasa katika Kubatiza.Ni katika kukiri ubatizo wa Kristo tunamkiri, tunamsadiki na kumfuasa Kristo. Tukiwa na Kristo maisha yetu yanapata auheni. Kristo ndiye mwenye kutuimarisha katika maisha yetu. Muunganiko wetu na Kristo hutufanya tuuone uso wa Mungu Baba, hutufanya tuurithi ufalme wa Mbinguni. Wahenga husema ,"watu wenye kufanana hutembea pamoja", Muunganiko wetu na Kristu ni katika kutembea na Kristo. Ufuasi wetu kwa Kristo ni kuwa tayari naye licha ya changamoto zetu za maisha, kwani aliye tayari¹ kumfuata ndiye mwenye kuuchukua msalaba wake.
Sala Ee Yesu Kristo, tunakukiri kuwa wewe ndiye mwokozi wetu, tunajinyenyekeza mbele yako na tunakuja mbele yako, daima tuongoze maishani ili tuweze kuupata uzima wa milele Amina
@ Claretian Publication