MUNGU ANA HAJA NASI KATIKA HALI YOYOTE YA MAISHA YETU
Katika Ukombozi wa Waisraeli, Mungu ana haja na Sauli mwana wa Kishi. Ssuli ameishi maisha ya kawaida , ametumwa na baba yake pamoja na mtumishi wake mmoja waende wakatafute punda. Naye hajakataa kuungana na mtumishi, hajakataa kwenda kutafuta punda . Ndipo katika hali yake hiyo ya kawaida anateuliwa na Bwana kuwaongoza watu wake.
Katika Injili Takatifu, yesu anamwita Lawi aliyeketi forodhani , pia anakula na watoza ushuru na wadhambi , jambo linalowashangaza waandishi na Mafarisayo.Yesu ana haja na Lawi , ana haja na watoza ushuru na wadhambi walioonekana wadhaifu na wasiofaa katika jamii yao. Hawa wanahitaji huruma na msamaha wa Yesu, ndio tiba kwao. Katika maisha yetu inawezekana tukawa watu tunaojiona hatustahili, ama wengine kadiri ya mienendo yetu tukaonekana hatufai kabisa lakini Mungu ana haja nasi jinsi tulivyo; hivyo tusijidharau , tusijipige vita, tusiwadharau wengine. Daima Bwana anatuhitaji wadhambi twende kwake , na tumuendee hasa kwa Sakramenti ya kitubio.
Sala
Ee Mungu utujalie kuwa karibu nawe hata katika madhaifu yetu. Amina
@ Claretian Publication