TUMECHAGULIWA KUIENEZA HABARI NJEMA KWA WATU WOTE
Katika sikukuu hii ya kuongoka kwa Mtakatifu Paulo Mtume, tunashuhuduwa na Mtume Paulo mwenyewe , jinsi slivyoitwa na kuongoka . Mtume Paulo kabla ya kuongoka alikuwa akiwatesa Wakristo kutokana na kusimamia dini na Sheria za Kiyahudi, baadae anapata maono na anatumwa na Kristo.Mtume Paulo anauliza jambo la kufanya na anaelekezwa .Anania anamweleza juu ya kuchaguliwa kwake na kwamba na kwamba atamshuhudia Mungu kwa watu wote. Katika injili tunamuona Yesu Kristo akiwatuma mitume kumi na mmoja, wakaihubiri Habari Njema kwa kila kiumbe.Taifa la Mungu, kwa ubatizo wetu tumechaguliwa na tunafanywa Wakristo na Sakramenti ya Kipaimara tunapokea nguvu ya Roho Mtakatifu, ili tuwe askari hodari wa Kristo na kumshuhudia kwa mawazo, maneno na matendo yetu.
Sala
Ee Mungu utujalie neema ya kuwa mashuhuda wa Injili yako. Amina