UNYOFU WA MAISHA NI UFUASI WA KWELI KWA KRISTO;
Wanafunzi wa Yohane na Mafarisayo walifunga, lakini namna yao ya kufunga ni ya kujionyesha , ni kufuata sheria . Wao wanafanya hivyo ili kupata sifa za Kibinadamu machoni pa watu. Jibu la Yesu kwao ni kuwaashiria kuwa ufuasi wa kweli ni katika unyofu mbele ya Mungu na si kutaka kuonekana kwa watu . Yesu Kristo ndiye Bwana arusi kumbe wanafunzi wake hawana haja ya kufunga kwa kuwapendezesha wanadamu ikiwa wapo na Mwokozi wao. Samweli anamkumbusha Sauli juu ya kutokuwa mnyofu mbele ya Mungu kwa kukosa utii, amemuasi Bwana kwa kulikataa Neno lake. Wapendwa, katika maisha yetu unyofu wetu ndio uhai wa Ukristo wetu. Katka kumfuasa Kristo tusifanye mambo ili kupata sifa za Kibinadamu, bali tufanye kwa sifa na utukufu wa Mungu. Haya huwezekana kwa kuwa watii na kulisikiliza Neno la Bwana.
Sala Ee Bwana tunakuomba utujalie unyofu wa maisha yetu katika kukufuata wewe , ili popote tunapokuwa tuweze kudhihirisha kazi yako katika maisha yetu Amina
@ Claretian Publication