SHERIA ZITUPONYE NA SIO KUTUANGAMIZA
Injili Takatifu inadhihirisha namna Mafarisayo walivyo watumwa wa sheria kiasi kwamba kwao ni vigumu kuthamini uhai wa watu. Yesu anawakumbusha kuwa taratibu zetu za maisha tunazojiwekea ni kwa ajili ya wokovu wetu. Wokovu wetu ndio thamani yetu mbele ya Mungu. Thamani hii haitokani na kufuata sheria tu, bali kutambua umuhimu wa sheria hizo na kuzitumia vema kadiri ya mpango wa Mungu. Thamani ya Waisraeli mbele za Mungu ndio inapelekea kuinuliwa kwa mfalme mwingine badala ya Sauli . Bwana anapendezwa nasi kwa kuona tunafuata taratibu, Sheria na amri kwa ajili ya wokovu wetu. Katika jamii zetu tumeweza kushuhudia kauli mbalimbali ambazo daima zinadhihirisha kipaumbele chetu katika matakwa yetu zaidi kuliko ya Mungu, kwa mfano tunasikia ," Ameuawa na watu wasiojulikana, Waliomuua wamejichukulia sheria mkononi, mara ukiingia kwenye kumi na nane huponi,nk". Namna kama hizi zinapaswa kukwepwa.Daima sheria zetu zituponye, ziturekebishe, zitupeleke kwa Mungu.
Sala Ee Mungu Mwenyezi wanao tunakuja mbele yako tukiomba maongozi yako katika kutambua thamani ya utu wa wenzetu kuliko kushikilia sheria tu Amina
@ Claretian Publication