KWA MUNGU KUNA KITULIZO CHA KWELI
Mwanariadha yeyote, daima hufanya mazoezi ya kutosha ili kuupa mwili wake uwezo wa kuhimili changamoto zozote zile, wakati wa mashindano. Tegemeo lake liko katika uwezo wake wa kupumua (pumzi), na uwezo wa misuli kumbeba kwenye muda wa mbio zenyewe. Pia yeye hutumainia kuwa miguu itaweza kumbeba kwa kasi hata aweze kuwapiku wenzake. Uwezo wake wa pumzi ndio unaomwezesha kukimbia umbali mrefu bila kuchoka na kwa mafanikio. Somo la kwanza na Injili ya leo zinazungumzia ujumbe kama huu. Isaya anatuambia, “Bwana Mungu hachoki, daima ana nguvu mpya, na ya kuwa wanaomtegemea daima watafanikiwa.” Mwinjili Matayo naye anasema kuwa Yesu anatualika daima tumtegemee yeye na sio kitu kingine kama vile mwanariadha anavyotegemea uwezo wa pumzi yake. Pumziko la kweli liko kwa Yesu. Tujifunze kutoka kwake kuwa na maisha ya unyenyekevu. Ni katika haya tunakuwa na maisha ya raha.
Sala Tunakuomba Bwana utuwezesha daima tukutegemee wewe na kimbilio letu daima liwe kwako. Amina
@Claretian Publication