Mtakatifu Timotheo
Mtakatifu Timotheo alizaliwa mwaka 17 huko Lystra, baba yake akiwa mgiriki na mama yake akiwa Myahudi, mkristo.
Muda ambao mtakatifu Paul alipoenda Lystra, tayari Timotheo alikuwa mkristo, na akawa rafiki yake. Na mtakatifu Paulo aliamua kushirikiana naye katika kazi zake za uinjilishaji. Na alifuatana nae katika safari yake ya pili. Mtakatifu Timotheo aliendelea kufanya kazi ,hata baada ya mtakatifu Paulo kuondoka.Alisafiri sehemu mbalimbali akiwapa moyo wakristo na kupeleka pia taarifa kwa mtakatifu Paulo. Hali hiyo ilimuwezesha mtakatifu Paulo kuandika nyaraka mbalimbali, kuwapa moyo wakristo, katika nyakati ngumu. Mwisho wake mtakatifu Timotheo alienda Efeso, ambako alikuwa askofu.Lakini baadae aliuwawa kwa kupigwa mawe , baada ya kukataa kushiriki katika ibada ya kipagani.Aliuwawa mwaka 97 huko Macedonia(Ugiriki ).
Mtakatifu Tito
Mtakatifu Tito, alikuwa na asili ya kigiriki. Na alisoma filosofia na mashahiri. Mtakatifu Tito alifanya kazi kumsaidia mtakatifu Paulo katika kazi mbalimbali, pamoja na kutafsiri. Na alifuatana nae katika safari yake kwenda katika mkutano huko Jerusalem. Wakati Mtakatifu Paulo alipotoka katika jela, huko Roma kwa mara ya kwanza, alienda katika kisiwa cha Crete kuhubiri. Na hapo, alimsimika Mtakatifu Tito kuwa Askofu wa Crete. Lakini baadae mtakatifu Paulo aliendelea kumuita , katika safari na kazi mbalimbali, katika sehemu tofauti. Mt Tito,Askofu, alikufa mwaka 96 huko Gortyn, Crete, Ugiriki.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Alberic ws Ceteaux
Mt. Ansurius
Mt. Athanasius
Mt. Conan
M/h. Michal Kozal
Mt. Paula
Mt. Robert wa Newmister
Mt. Theofrid
Mt. Thordgith
Watakatifu Timotheo Na Tito, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee....