Mtakatifu Gaspar
Mtakatifu Gaspar, mmoja kati ya Mamajusi watatu, alikuwa na asili ya India.Alikuwa msomi katika taaluma ya Unajimu.
Mtakatifu Gaspar alikuwa mtawala wa mji ambao alikuwa akiishi huko Kusini mwa India.
Mtakatifu Gaspar alileta zawadi ya Uvumba kwa ajili ya kuonyesha hadhi ya Umungu .
Alikutana na wenzake huko Armenia mwaka 54 ( Baada ya Kristu ) na akafa tarehe 11 Januari Mwaka 55, akiwa na miaka 109.
Baadae alizikwa huko Ujerumani katika Cathedral ya wafalme watatu huko Cologne, Pamoja na wenzake
Mtakatifu Melchior
Mtakatifu Melchior alikuwa na umri mkubwa kuliko wenzake wawili. Alikuwa pia mtawala katika Uajemi. Baada ya kufuata nyota na kufika Bethlehemu na kumuona mtoto Yesu alifungua zawadi yake (Dhahabu ) ishara ya Ufalme. Mtakatifu Melchior alikutana tena na wenzake ( Gaspar na Baltazar ) mwaka 54 Bk huko Armenia alipoenda kusheherekea Krismasi. Alikufa mwaka 56 Bk akiwa na miaka 116 , tarehe 1 Januari. Yeye na wenzake walizikwa pamoja huko Cologne Ujerumani, katika Cathedral ya wafalme watatu.
Mtakatifu Balthazar
Mtakatifu Balthazar alizaliwa mwaka 56 ( Kabla ya Kristu ) huko Macedonia. Alikuwa pia mtawala.
Mtakatifu Balthazar baada ya kumwona mtoto Yesu, naye pia alifungua zawadi ya Manemane, ambayo ilikuwa ni ishara ya Ubinadamu .Naye pia alikutana na wenzake huko Armenia katika sherehe ya kuzaliwa Bwana
Mtakatifu Balthazar alikufa mwaka 55 (Baada ya Kristu) akiwa na miaka 112.Naye pia alizikwa na wenzake huko Cologne Ujerumani katika Cathedral ya wafalme watatu.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Andre Bessette
Mt. Anastasius VIII
Mt. Diman
Mt. Edeyrn
Mt. Eigrad
Mt. Erminold
Mt. Hywyn
Mt. John de Ribera
Mt. Macra
Mt. Melanie
Mt. Melanius
Mt. Peter wa Canterbury
Mt. Schotin
Mt. Wiltrudis
Watakatifu Gaspar, Melchior Na Balthazar , Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...