Mtakatifu Flora
Mtakatifu Flora alizaliwa katika mji wa Cordoba, Hispania.Baba yakea akiwa muislamu na mama mkristo.Baba yake alikufa wakati akiwa bado mdogo.Hivyo alilelewa katika ukristo.
Kaka yake alijaribu kumwingiza katika dini ya kiislamu, hakufanikiwa.Akampeleka katika mamlaka iliyotawala mji ule, ambapo alifungwa na kupewa mwalimu wa elimu ya kiislamu ili kumfanya aache mafundisho ya kikristo. Akamudu kutoroka akienda sehemu ya mji, iliyokaliwa na wakristo.
Mtakatifu Mary
Mtakatifu Mary naye alizaliwa katika mji wa Elche, na baba mkristo na mama muislamu.Mama yake alibatizwa mara baada ya kuolewa.Familia yao, ikiwa na Mary na nduguye, walikimbilia katika mji wa Fronianus wakiepuka machafuko katika mji wa Elche.Mtakatifu Mary nae alifiwa na mama yake , akiwa mdogo.Baba yake aliamua kumpeleka katika nyumba ya masista ya Cuteclara.Kaka yake mtakatifu Mary aliyeitwa Walabonsus, naye alipata elimu ya dini katika kituo cha watawa cha mtakatifu Felix.Walikuja kuonana tena kaka huyo alipchaguliwa kuwa mmoja wa wasimamizi wa convent ambayo Mary alikuwepo.Kaka huyo nae alikatwa kichwa na watawala wa kiislamu tarehe 16 Julai 851.
Watakatifu Mary na Flora walikutana katika kanisa la mtakatifu Acisclus, wakakubaliana kuukataa uislamu pamoja.Walifanya hivyo mbele ya kadhi , wakahukumiwa kufungwa. Wakiwa jela , mtakatifu Flora alihaidiwa msamaha kama akirudi katika uislamu.Alikataa akiwaeleza kuwa anaamini katika ukristo tu. Kulingana na sharia, Flora na Mary walipatikana na hatia ya makosa mawili, wakahukumiwa kifo.Walikatwa vichwa tarehe 24 Novemba 851.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Andrew Dung Lac
Mt. Alexander
Mt. Anthony Nam-Quynh
Mt. Bernard Due
Mt. Bieuzy
Mt. Chrysogonus
Mt. Colman wa Cloyne
Mt. Columbanus
Mt. Crescentian
Mt. Eanfleda
Mt. Felicissimus
Mt. Firmina
Mt. Joachim Ho
Mt. Kenan
Bl. Lawrence PeMan
Mt. Leopardinus
Bl. Maria Anna Sala
Mt. Marinus
Mashahidi wa shirika la Dominican wa Vietnam
Mt. Eanfleda
Mt. Felicissimus
Mt. Firmina
Mt. Joachim Ho
Mt. Kenan
M/h. Lawrence PeMan
Mt. Leopardinus
M/h. Maria Anna Sala
Mt. Marinus
Mashahidi wa Dominican, Vietnam
Wt. Peter Domoulin Bori, Peter Khoa, na Vincent Diem
Mt. Romanus wa Le Mans
Mt. Stephen Theodore Cuenot
Mt. Stephen Vinh
M/h. Thaddeus Lieu
Mt. Theophane Venard
Mt. Thephane Venard
Mt. Vicente Liem de la Paz
Watakatifu Flora Na Mary, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote wa Leo, Mtuombee.....