Mwenye heri Urban V ,alizaliwa mwaka 1310 huko Grizac,Languedoc-Roussillon, Ufaransa. Akabatizwa Guillaume de Grimoard.
Guillaume alisoma huko Montpellier na Toulouse, akajiunga na wa Benedictine huko Marseilles. Akapata daaraja la Upadri mwaka 1334 huko Chirac.
Akapata pia udaktari wa sheria,na akawa Abate katika manosteri ya St German, huko Auxerre na St Victor huko Marseilles.
Mwaka 1352 Papa Clement VI alimuita Guillaume huko Roma kwa kazi maalum
Mwaka 1354,Guillaume aliitwa tena na Papa kwa kazi maalum tena.Papa alimuita tena mwaka 1362 kusaidia shughuli za utawala katika baadhi ya majimbo, huko Italia.
Papa Innocent VI, alikufa tarehe 12 September 1362,na tarehe 22 mwezi huohuo baraza (conclave )lilikaa kwa ajili ya kuchagua Papa.Tarehe 28 September 1362, Abate Guillaume de Grimoard alichaguliwa kuwa Papa ,akachukua jina la Urban V.
Papa Urban V, alifanya kazi nyingi njema, akaanzisha vyuo Vikuu katika miji mbalimbali .Akatembelea miji mbalimbali katika kuinjilisha na kuelimisha wapinga Kristo.
Papa Urban V, alikufa mwaka 1372, huko Avignon, Italia.Alitangazwa mwenye heri mwaka 1870 March 10 na Papa Pius IX .
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Nemesius
Mt. Anastasius I
Mt. Augustine Moi
Mt. Bernard Valeara
Mt. Darius
Mt. Dominic Uy
Mt. Fausta
M/h. Francis Man
Mt. Francis Xavier Mau
Mt. Manirus
Wt. Meuris na Thea
Mt. Nemesius wa Alexandria
Mt. Ribert
Mt. Thomas De na wenzake
Mwenye Heri Urban, Wenyeheri Na Watakatifu Wote Wa Leo, Mtuombee....