Mtakatifu Yohane alizaliwa huko Bethsaida Galilaya katika karne ya kwanza. Alikuwa mwana wa Zebedayo na Salome. Mtakatifu Yohane, alikuwa mmoja kati ya mitume 12 wa Yesu. Alikuwa pia na nduguye aliyeitwa Yakobo . Mtakatifu Yohane na Yakobo pamoja na Petro walishuhudia Yesu akimfufua binti wa Yairo.
Mtakatifu Yohane, alikuwepo msalabani akiwa na mama Maria, wakati Bwana Yesu aliposulibishwa.
Baada ya Bwana kupaa mbinguni,Mtakatifu Yohane alienda katika nchi ya Waefeso na baadaye akaishi katika kisiwa cha Patmos ambako aliandika kitabu cha Ufunuo.
Mtakatifu Yohane alikufa mwaka 100 (baada ya Kristo ), katika kisiwa cha Patmos, Ugiriki.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Fabiola
Mt. Maximus
Mt. Nicarete
Wt. Theodore na Theophanes
Mtakatifu Yohane, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...