Mtakatifu Yasinta, alizaliwa mwaka 1585 March 16, huko Vignanello - Viterbo, Italia.Alizaliwa katika familia njema yenye uwezo kiuchumi.Alipobatizwa aliitwa Clarice.
Akiwa na mdogo, yeye na dada yake walipelekwa katika shule ya manosteri ya mtakatifu Bernardino, ambako walisimamiwa na watawa wa Franciscan, wa utawa wa tatu. Baada ya elimu ,Dada yake aliamua kuwa mtawa, lakini Mtakatifu Yasinta aliamua kurudi katika maisha ya kawaida.Lakini pia akiwa mjeuri na mwenye kiburi. Akiwa na miaka 20, aliposwa na kijana aliyeitwa Marchese Capizucchi.Lakini kijana huyo alimuacha na kumuoa mdogo wake aliyeitwa Ortensia.Jambo hilo lilimvunja moyo mno, na akaamua kujiunga na shirika la Wa Franciscan, katika manosteri ya Viterbo. Hapo ndipo alipochukua jina la Yasinta.
Lakini bado aliendelea kujiwekea vitu vingi, chakula cha ziada na nguo na vitu vya thamani.Lakini siku moja , akiwa mgonjwa sana, alihitaji Padri kwa ajiri ya maungamo na komunio.Padri alishangazwa na muonekano wa chumba cha Mtakatifu Yasinta. Padri huyo alimueleza jinsi ya kuishi vizuri, akiwa mtawa. Mtakatifu Yasinta alifuata maelekezo ya Padri, akagawa vitu vyote alivyoweka chumbani kwake.Akivaa nguo iliyochakaa, akitembea bila viatu, na maisha ya majitoleo.
Mtakatifu Yasinta, aliishi maisha ya sala, na majitoleo. Alisaidia wenye shida, mpaka alipokufa mwaka 1640 Januari 30 huko Viterbo Italia. Alitangazwa mwenye heri mwaka 1726 na Papa Benedict XIII, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1807 May 14 na Papa Pius VII.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Aldegunais
Mt. Aleaunie
Mt. Alexander
Mt. Armentarius
Mt. Barsimaeus
Mt. Bathildis
Mt. Felician
Mt. Hippolytus
Mt. Martina wa Rome
Mt. Matthias wa Jerusalem
Mt. Mutien-Marie Wiaux
Mt. Savina wa Milan
Mt. Tudy
Mtakatifu Yasinta, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee..