Mtakatifu Winebald, alizaliwa mwaka 701, huko West Saxon, Uingereza. Baba yake alikuwa mtakatifu Richard. Alikuwa pia kaka wa mtakatifu Willibald, na dada yao Mtakatifu Walburga.
Mwaka 721 Mtakatifu Winebald akiwa na baba yake na nduguye, waliondoka kwenda kuhiji katika mji wa Roma.Baba yao (Mtakatifu Richard )aliugua na kufa nchini Italia. Mtakatifu Winebald aliamua kubaki Roma kwa masomo zaidi.
Mwaka 739, Mtakatifu Boniface alienda Roma na akampangia mtakatifu Winebald kwenda kufanya Umisionari huko Ujerumani. Akampa daraja la upadri na kumpa usimamizi wa makanisa katika Ujerumani na Bavaria.
Kaka yake (mtakatifu Willibald) tayari alikuwa askofu wa Eichstatt alimuomba nduguye kuanzisha manosteri na seminari, kwa ajiri ya kufundisha mapadri. Lakini kutokana na afya yake kuwa dhaifu, hakufanya hivyo.Lakini dada yake (mtakatifu Walburga ) alitoka kwao Uingereza na kwenda Heidenheim. Hapo alianzisha manosteri na convent ya masista, ambao walifuata sheria ya wa Benedictine.
Mtakatifu Winebald alikufa mwaka 761, Desemba 18 huko Heidenheim, Ujerumani.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Joseph wa Cupertino
Mt. Basilides
M/h. Carlo Erana Guruceta
Mt. Dominic Trach
Mt. Eumenes
Mt. Ferreolus
Mt. Hygbald
M/h. Jesus Hita Miranda
Mt. John Macias
Mt. Ludmilla wa Bohemia
Mt. Methodius wa Olympus
Mt. Richardis
Mtakatifu Winebald, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee....