Mtakatifu Thomas Becket alizaliwa mwaka 1119 Desemba 21, huko Cheapside, London, Uingereza. Alisoma masomo ya awali katika shule ya Merton Priory huko Sussex, na baadae chuo kikuu cha Paris.
Aliporudi London,alifanya kazi ya karani wa mahakama ,na alipofika miaka 24, alipewa kazi katika makazi ya Theobald, ambaye alikuwa Askofu mkuu wa Canterbury.
Kwa ruhusa ya Askofu, mtakatifu Thomas alisoma sheria za kanisa katika chuo kikuu cha Bologna huko Hispania na kuendelea katika chuo kikuu cha Auxerre, huko Ufaransa.
Mwaka 1154 alipata daraja la ushemasi, akitumika kama shemasi mkuu .Mwaka 1161 Askofu mkuu Theobald alikufa.Mwezi Mei mwaka 1162,Mtakatifu Thomas akachaguliwa kuwa Askofu, akapewa kwanza daraja la upadri mwaka 1162 June 2, na kesho yake June 3, akasimikwa kuwa Askofu . Akawa Askofu wa Canterbury, japo alifahamu kuwa kwa kuzingatia misingi ya kanisa, asingelewana na mtawala wa Uingereza wakati huo.
Na kutokana na misimamo yake thabiti ya kufuata taratibu za kanisa, akiwa kama Askofu, alikosana na mfalme, na kukosa kukubaliana nae mambo mengi.
Mtakatifu Thomas Becket aliuwawa kanisani katika cathedral ya Canterbury na askari waliotumwa na mfalme, mwaka 1170, Desemba 29, na akazikwa humo humo katika Cathedral ya Canterbury.
Mtakatifu Thomas Becket alitangazwa mwenye heri mwaka 1173 February 21 na kutangazwa mtakatifu siku hiyo hiyo na Papa Alexander III.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Aileran
Mt. Albert wa Gambron
Wt. Callistus, Felix na Boniface
Mt. Dominic
Mt. Ebrulf
Mt. Trophimus of Arles
M/h. William Howard
Mtakatifu Thomas, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee....