Mtakatifu Theodosius alizaliwa mwaka 423, huko Cappadocia (Uturuki ).Akasafiri kwenda kuhiji Jerusalem, ambapo alikutana na mtakatifu Simeon wa Mnarani. Akaamua kuingia maisha ya utawa.
Akaenda kuishi maisha ya upweke, akisali na kuomba karibu na bahari nyekundu. Huko aliwavutia watu wengi, wengine wakaamua kuishi nae, katika maisha ya utawa.Akaanzisha Monasteri hapo.
Askofu wa Jerusalem akampa kazi mbalimbali, katika Palestina. Na Mtakatifu Theodosius akapata nafasi ya kuhubiri, akipinga mafundisho potofu ya wapinga Kristo.
Mtakatifu Theodosius alikufa Januari 11 529, huko Palestina.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Alexander
Mt. Anastasius X
Mt. Boadin
Mt. Brandan
Wt. Ethenea na Fidelmia
Mt. Francisca Salesia Aviat
Mt. Honorata
Mt. Hyginus, Papa
Mt. Leucius wa Brindisi
Mt. Palaemon
Wt. Paldo, Tato, na Taso
Mt. Paulinus wa Aquileia
Wt. Peter, Severus na Leucius
Mt. Salvius
Mt. Theodosius wa Antioch
Mt. Vitalis wa Gaza
M/h. William Carter
Mtakatifu Theodosius, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wa Leo, Mtuombee...