Mtakatifu Stefano alikuwa Mwisraeli, ambaye alikuwa na elimu ya kigiriki. Alichaguliwa kuwa shemasi, yeye na wenzake 6.Walichaguliwa na mitume wote kwa pamoja, ili kusaidia kufanya kazi ya Mungu kwa pamoja.
Mtakatifu Stefano alijaa hekima, na uelewa mkubwa. Mara nyingi alikuwa akishiriki katika kufundisha, na kuelekeza mambo yote yaliyokuwa na utatanishi wa kuelewa na pia kujibu maswali mbalimbali.
Katika moja ya mikutano yake, alikutana na kundi la Wayahudi, ambao walianza kumuuliza maswali mbalimbali, kutoka katika maandiko matakatifu. Wayahudi hao, baada ya kuzidiwa busara na Mtakatifu Stefano, walimzulia tuhuma za uongo, kwamba alimkufuru Mungu.
Wakamuhukumu kufa, kwa kumpiga na mawe. (Mat.7:51-53)
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Abadiu
Mt. Amaethlu
Mt. Archelaus
Mt. Papa Dionysius
Mt. Marinus
Mt. Neol Chabanel
Mt. Tathal
Mt. Theodore
Mt. Vincentia Maria Lopez Y Vicuna
Mt. Zeno
Mt. Zosimus
Mtakatifu Stefano, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee..